Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Baadhi ya Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Taasisi ya Diaspora ambao wapo Zanzibar kutoa huduma za Afya bure kwa muda wa siku Tano.
Balozi Seif kulia akibadilishana mawazo na Kiongozi wa Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Taasisi ya Diaspora Bibi Asha Nyang’anyi mwenye asili ya Tanzania.
Balozi Seif kati kati akizungumza na Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Taasisi ya Diaspora waliopo Zanzibar kutoa huduma za Afya katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Kiongozi wa Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Taasisi ya Diaspora Bibi Asha Nyang’anyi mwenye asili ya Tanzania kati kati akifafanua jambo wakati Timu yake ilipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kiongozi wa Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Taasisi ya Diaspora Bibi Asha Nyang’anyi Kulia akimkabidhi Balozi Seif baadhi ya Vifaa na Dawa zitakazotumika wakati wanapotoa huduma za Afya.
Balozi Seif aliyepo kati kati waliokaa vitini akiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Taasisi ya Diaspora waliopo Zanzibar kutoa huduma za Afya.
Balosi Seif Kushoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mahesabu cha Taasisi ya Headinc ilichounda Timu ya Madaktari na Wauguzi kutoka Nchini Marekani kupitia Diaspora Bwana Iddi Sandaly.(Picha na – OMPR – ZNZ.)
Na. Othman Khmais OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaelewa na kutambua umuhimu wa Taasisi zinazojumuisha Watanzania walioko nje ya Nchi zenye utararibu wa kuchangia maendeleo ya Uchumi na Kijamii kupitia misaada na huduma mbali mbali.
Alisema umuhimu huo umepelekea Serikali kuunda Idara ya Uratibu ya Wazanzibar wanaoishi nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa ili kuzipa nguvu Taasisi hizo ikilenga zaidi ile ya Diaspora.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Timu ya Madaktari, Wataalamu wa Sekta ya Afya pamoja na Wauguzi kutoka Nchini Marekani wanaounda Timu ya Diaspora ambao wapo Zanzibar kutoa huduma mbali mbali za Afya bure katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja katika kipindi cha siku Tano kilichoanzia Jumatatu.
Alisema azma ya Timu hiyo ya Madaktari ya kusogeza huduma za Kijamii kwa Wananchi wa rika zote Visiwani Zanzibar imeleta faraja kubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyojipanga kuimarisha huduma za Afya katika kila masafa yasiyopungua Kilomita Tano.
“ Sera ya Afya Zanzibar ni kuwa na Vituo vya Afya kila baada ya kilomita Tano ili kuwaondoshea shiha ya kupata huduima hiyo Wananchi hasa Vijijini”. Alifafanua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif aliihakikishia Tumu hiyo ya Madaktari kutoka Marekani chini ya Mwamvuli wa Diaspora kwamba Serikali Kuu itaendelea kushirikiana nao katika kuona malengo waliyojipangia yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo Balozi Seif aliwaasa wananchama wa Jumuiya hiyo ya Diaspora wale wenye asili ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kukunjua zaidi mikono yao katika kusaidia Jamii yao ili faida ya uwepo wao nje ya Nchi uweze kuleta tija.
Alisema ni vyema masuala hayo yakaenda sambamba kwa Wanachama hao kuangalia hatma ya maisha yao ya baadae wakielewa kwamba Nyumbani kutabakia muhimu kwao katika maisha yao ya baadae.
Mapema Kiongozi wa Timu ya Madaktari hao Kutoka Nchini Marekani wa Diaspora mwenye asili ya Tanzania Mtaalamu wa Maabara Asha Nyang’anyi alisema Timu yake imejipanga kutoka Huduma za Afya Zanzibar kwa Wananchi wa rika zote.
Bibi Asha alisema uwepo wao Nchini utatoa fursa kwa watu mbali mbali kuchunguzwa afya zao hasa katika maradhi ya Ngozi, Shindikizo la Damu. Kisukari pamoja na afya ya akina Mama.
Alisema uwamuzi wao huo umekuja baada ya washirika wa Taasisi hiyo kutoka Nchi mbali mbali Duniani hasa zile za Bara la Afrika wanaoishi Nchini Marekani kujikusanya pamoja wakilenga kusaidia Jamii ya Nchi zitakazohitaji huduma za Kijamii ambazo ziko ndani ya uwezo wao.
Timu hiyo ya Madaktari, Wataalamu wa Sekta ya Afya pamoja na Wauguzi kutoka Nchini Marekani wanaounda Timu ya Diaspora wana asili ya Mataifa ya Nigeria, Cameroun, Lesotho, Norway, Canada na wengi wao ni Watanzania.
3 comments:
This is photo OP I don't think will make sense for a short visit to TZ will help to solve those patients problems.In a good faith they need to send money, medical equipment and medication to some hospitals of their choice to help poor Tanzanians to get free and better medical services. Because, TZ have excellent Doctors who can treat those sick people for less than bringing delegation of 20 people from USA to TZ. Money spent on air tickets and living expenses, would help many patients and for a long time. Advise to Tanzanians who want to do good stuff back home let us think outside the box first.
You can't solve all the problem,but you can be part of the solution.Actually,I support that group for going to Znz and volunteer their time and money.In a big picture,Govt of Tz has responsibility of buy medicines and medical equipments.That group can spend money anyway in airline tickets for their own vacation back home if they choose to do so.Lets think positive and support each other.
Absolutely! Agree 100%. Funds can be used more efficiently and strategically than on team travel.
Post a Comment