Bodi ya Wadhamini iliyo chini ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, imeiomba Mahakama Kuu iitendee haki kwa kuithibitisha kama bodi halali ya chama hicho, ili iweze kufuta kesi zilizofunguliwa dhidi ya Lipumba na wenzake, kwa madai zilifunguliwa na Bodi isiyo halali.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari, jana Julai 6, 2017 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Slaam , Katibu wa Bodi hiyo, Thomas Malima alidai kuwa mahakama hiyo haikuwatendea haki kwa kutothibitisha uhalali wa bodi hiyo pamoja na kutowatambua mawakili wake.
Aidha, Bodi ya Wadhamini iliyo chini ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad imefungua mashauri takribani sita dhidi ya Lipumba na wenzake ikiwemo shauri la kuzuia utolewaji wa fedha za rudhuku ya chama hicho kwa Lipumba.
Na kwamba Bodi ya Lipumba inadai kuwa kesi hizo zimefunguliwa kinyume na sheria kwa kuwa yenyewe ndiyo yenye uhalali wa kufungua kesi za chama hicho.
No comments:
Post a Comment