ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 8, 2017

MANISPAA YA ILALA YATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25 KWA KUTOHUDUMIA IPASAVYO DAMPO LA PUGU KINYAMWEZI.

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akionyesha jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema hii jijini Dar es salaam ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Wilaya ya Ilala.   
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akiwa ameambatana na Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi ambapo ameipiga faini ya milioni 25 Manispaa ya Ilala kwa uchafu wa mazingira kwa wakazi wa Pugu.    
 
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizumgumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo aliyoifanya katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Ilala jijini Dar es salaam.   
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akibadiishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(katikati), Sophia Mjema na kushoto ni Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita wakati wa ziara ya ukaguzi wa uchafuzi wa mazingira uliofanyia katika dampo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es salaam.  

NA; EVELYN MKOKOI
Kufuatia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, iliyofanyika Jijini Dar es Salam katika Manispaa ya Ilala, ilohusisha ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkaguzi wa Mazingira wa kanda ya Mashariki Bw. Jaffari Chimgege, limeitoza faini Manispaa  ya jiji ya Dar es Salaam kiasi cha shilingi Milioni 25, kwa kosa la uchafuzi wa Mazingira wa kutohudumia Dampo hilo ipasavyo na kupelekea harufu mbaya, vumbi na maji yenye sumu kali  na kuhatarisha afya ya wakazi wa maeneo jirani viumbe hai na mzingira kwa ujumla.
Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Viwege uliyopo katika kata ya Majoe yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bi Amina Rashid yaliyoeleza kuwa na changamoto mbali mbali katika dampo hilo zikiwemo za vumbi na maji yenye kemikali kwenda katika maeneo ya makazi, Naibu Waziri Mpina, ameitaka Halmashauri ya jiji kuja na mpango mkakati utakaoweza kuupunguzia mzigo dampo la Pugu ambalo kwa sasa linatumika kupokea takataka zote za Halmashauri za jiji la Dar es Salaam na kuonekana kulemewa na mpango huo uwezeshe kila manispaa kuwa na dampo lake.
Aidha Mpina alibaini kuwepo kwa madhaifu makubwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kuondosha taka katika manispaa za jiji na kuutaka uongozi wa jiji Hususan Mkurugenzi wa Jiji kufuatilia madeni hayo kikamilifu, pamoja na kutoa deadline ya uwasilishwaji wa fedha hizo “ni vyema ghahama za uondoshwaji wa taka zikatokana na taka zenyewe na siyo kutoa fedha za kuhudumia taka kutoka katika vyanzo vingine vya mapato. Alisisitiza Mpina.”
Mpina pia aliitaka manispaa ya jiji  kutafuta namna bora ya kuondosha taka sumu na kuelekeza taka zote za matairi katika jiji la Dar es Salaam zitafutiwe sehemu tofauti na namna pekee ya kuzitekekeza.
Akionekana kuongea kwa hasira na msisitizo Naibu Waziri Mpina alisema, “ Hakuna kitu nisichopenda katika utendaji wangu kama kuona taasisi za serikali zikiwa za kwanza katika suala zima la uchafuzi wa mazingira, faini hiyo jiji mtailipa ndani ya siku 14, na kuhakikisha mnarekebisha  matobo yote yanayolalamikiwa kupitisha maji na kupeleka katika makazi ya wananchi pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua, na maji ya sumu yaende katika mkondo sahihi wa maji hatarishi na bila kusahau kuruhsu maji hayo baada ya kujiridhisha na vipimo vinavyotakiwa.
Awali akitoa taarifa ya hali ya mazingira  na usimamizi wa taka katika Dampo  la Pugu Kinyamwezi , Mkuu wa Idara ya usimamizi taka wa jiji la hilo Bw. Shedrack Maximillian alimueleza Mpina kuwa jiji linakabiliana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja dampo kupata moto, dampo kutokuwa la kisasa na maji yenye sumu kwenda katika makazi ya wananchi.
Hata hivyo Manispaa ya ilala imetenga kiasi cha fedha shilingi Bilioni moja za kitanzania kwa mwaka wa fedha ulioisha pamoja na kuzungumza na wadau wa maendeleo ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuweza kuboresha Dampo hilo kinalotumika kwa kiasi kikubwa na manispaa zote za jiji la Dar es Salaam.

No comments: