Sauda Karoli
Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amefunguka kwa kudai kuwa siku ya show yake ya Miaka 15 ya Saida Karoli itayofanyika weekend hii katika ukumbi wa Escape One jijini Dar es salaam ataachia albamu yake ya ‘Best Of Sauda Karoli’.
Akiongea Jumanne hii, Saida amedai albamu hiyo itakuwa na nyimbo nyingi mpya pamoja zile za zamani ambazo zilifanya vizuri kipindi cha nyuma.
“Alhamisi nataka kuwaonyesha nilichokuwa nafanya wakati nimeanguka na nilichokipata huko, nimejiandaa vya kutosha kwaajili ya kazi tu,” alisema Saida. “Pia siku hiyo nitazindua albamu yangu mpya ‘Best Of Saida Karoli’ na itakuwa na nyimbo za zamani na mpya, kwahiyo sio kitu chakukosa kabisa,”
Muimbaji huyo alikuwa kimya kwa muda mrefu kwenye muziki kabla ya kurudi upya na wimbo ‘Orugambo’ ambao ndani yake una vionjo vya wimbo wa Diamond na Belle 9.
No comments:
Post a Comment