ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 7, 2017

TPB BANK YAIPA SERIKALI GAWIO LA BILIONI 1

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi Hundi kifani yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.032/- Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Phillip Mpango. Gawio hilo limetolewa kwa Serikali baada ya benki hiyo kupata faida ya shilingi Bilioni 15 mwaka jana. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi. Tukio hilo ilifanyika kwenye Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango , Dodoma
 Wakishika kwa pamoja mfano huo wa hundi baada ya makabidhiano.
KWA mara ya kwanza, TPB Bank PLC, jana imetoa gawiwo kwa Serikali huku Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akionya taasisi za fedha ambazo zinafanya utatakitishaji wa fedha hazitafumbiwa macho.


TPB Bank PLC ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 86.17 imekabidhi gawio la fedha taslimu la Sh bilioni 1.032 huku mwanahisa mwingine Shirika la Posta likigawiwa Sh milioni 97 wakati wanahisa wengine Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na na Posta na Simu Saccos zikipewa gawio la hisa.


Akizungumza mara baada ya kupokea hudi, Mpango aliipongeza Benki ya TPB kwa mafanikio yaliyopelekea kuipatia Serikali gawio hilo kwa mara ya kwanza. 

“Niwapongeze kwa mfanikio, niwasihi ninyi kama benki ya umma mkajitumbukiza kwenye kashafa za kutakatisha fedha. Taasisi zitakazofanya miamala ya hovyo hvyo hatutasita kuchukua hatua kwa wanaosababisha hasara kubwa kwa nchi, sasa timetosha.


 Akizungumzia hatua ya TPB Bank kutoa gawio kwa serikali, alisema inatia moyo kwa taasisi ambazo serikali imewekeza zikilipa kodi na kutoa gaiwo kwani fedha hizo ndizo zinazotumika kuwahudumia wananchi.


“Kuna vitu ambavyo havipendezi hata kidogo, watoto wanakaa chini, kuna wazee ambao wamelitumikia taifa hili, lakini tunashindwa kuwahudumia hata kwa kutoa matibabu kwa bure, na ni watu ambao kama wao wasingejituma uwenda sisi tusingekuwepo.


Aidha, Mpango aliutaka uongozi wa TPB Bank kuhakikisha wanakuja na mfumo wa kusaidia Wanawake na wajasiliamali wadogo kuweza kupata mitaji kwani ndio makundi makubwa yenye uhitaji mkubwa wa mitaji na kuwa wakiwezeswa wanaweza kusaidia katika harakati za kukuza uchumi.


“Serikali inadhamira ya kweli katika kuwawezesha watanzania kiuchumi kwani nia ni kufikia uchumi wa kati si kwa tarakimu bali utakaogusa moja kwa moja wananchi, hivyo ninyi mnanafasi ya kuwafikia hawa wajasiliamali ambao ambao ndio wahitaji wakubwa.


Naye Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema kwa mara ya kwanza benki yake imetoa gawio kwa wanahisa pamoja na kuwa na tataizo la kimtaji.


“Niliikuta benki inajiendesha kwa hasara, lakini baada ya mabaliko hayo mwaka 2011 tulianza kuzalisha faida lakini kwa muda wote tulikuwa tunaomba wanahisa kutumia fadia hiyo kuimarisha mtaji,” alisema.

No comments: