ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 9, 2017

GRAÇA MACHEL AWATAKA WAJITUME WAJITUME


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza kwenye mkutano wa ana kwa ana na wanawake mashujaa uliofanyika leo kwenye ukumbi wa hoteli ya Haytt leo jijini Dar es Salaam.

Alikuwa mke wa marehemu Rais wa Msumbiji, Graça Machel akizungumza na wanawake kuhusu namna ya mwanamke kujiamini pamoja na kufanya kazi ka bidii ili kufikia malengo aliyojiwekea kwenye mkutano ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na taasisi ya GRACE  MACHEL FOUNDATION ya  nchini Afrika Kusini.


Zaidi ya washiriki 60 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wamekutana leo jijini Dar es Salaam katika tukio la ana kwa ana na wanawake mashujaa likiwa na lengo la kujadili na kuangalia changamoto zinazowakabili wanawake.
Tukio hilo limeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na taasisi ya GRACE  MACHEL FOUNDATION ya  nchini Afrika kusini ambayo inajishughulisha na shughuli zake barani Afrika ambalo litafanyika kwa siku nne.
Akizungumza katika tukio hilo mgeni rasmi Graça Machel amesema kuna haja ya kuangalia ni nini kinafanywa na wanawake na kuangalia uchumi wa mwanamke na umoja wa wanawake katika kutetea haki zao.
Naye Mama Gertrude Mongella akizungumza katika  tukio hilo amesema ili kuendana na kasi ya maendeleo kwa mwanamke hakuna haja ya mwanamke kulalamika, kuomba, kulia lia pamoja na kulaumu ili kuweza kuwapata wanawake wachapa kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi  amesema  wameamua kukutana pamoja ili kujitathmini huku wakiangalia agenda mbili ya wanawake na ukatili wa kijinsia pamoja na kuangalia haki ya uchumi na ushiriki wa wanawake katika uchumi.
Kupitia tukio hilo viongozi hao mashuhuri watapata nafasi ya kuulizwa maswali mbalimbali kutoka kwa washiriki wa tukio hilo ili washirikiki hao vijana na wao kuona kuwa inawezekana kufikia hatua walizofikia viongozi hao.
Akizungumza katika kongamano hilo kijana mwanaharakati kutoka Tanzania, Halima Lila amesema "Hatuna mwongozo sahihi wakulinda elimu ya mtoto wa kike,bado Kuna hitaji kubwa la kutoa elimu juu ya uzazi kwa vijana wakike na wa kiume" amesema.

Seif Ibrahim amesema Tanzania bado kuna tatizo la ajira kwa vijana na mimba kwa watoto wakike ambao wengi wanashindwa kumaliza elimu zao za sekondari lakini pia elimu zinazotolewa kwa vijana mashuleni haziwapi uwezo wa kujitegemea wamalizapo masomo "amesema.
Mama Gertrude Mongella(katikati)  akiwasisitiza wanamke kuwa hakuna haja ya mwanamke kulalamika, kuomba, kulia lia pamoja na kulaumu ili kuweza kuwapata wanawake wachapa kazi kwenye mkutano uliowakutanisha wanawake mashuuri hapa barani Afrika.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama akizungumza jambo kwa wanawake waliofika kwenye kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam
Prof. Ruth Meena akiwasilisha mada kwa wanawake pamoja na viongozi na baadhi ya wanawake mashujaa wa barani Afrika waliofika kwenye kongamano la uso kwa uso lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Dk. Gennet Zewide

Baadhi ya wanawake waliofika kwenye kongamano hilo wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwenye kongamano hilo lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Picha ya Pamoja

No comments: