ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 31, 2017

LIBYA YAIPATIA ZANZIBAR MSAADA WA MATREKTA


Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania, Bw. Saleh Kusa Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam leo. Wawili hao walijadili namna ya kukamilisha taratibu za kukabidhi msaada wa matrekta 10 yenye thamani ya zaidi ya milioni 250 za Tanzania kutoka Libya kwa ajili ya Serikali ya Zanzibar. Matrekta hayo yashawasili jijini Dar es Salaam na wiki ijayo yanatarajiwa kukabidhiwa Serikali ya Zanzibar. Aidha, Kaimu Balozi alisema kuwa Libya imetenga Dola Bilioni 20 kupitia Mfuko wa "Libyan-Africa Investment Portfolio" kwa ajili ya nchi za Afrika. Aliahidi kuwa atahakikisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zinaletwa Tanzania.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Saleh na Afisa Dawati wa Libya, Bw. Nicolas wakifuatilia mazungumzo

Kulia ni Mkalimani wa Kaimu Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Serikali ya Zanzibar wakifuatilia mazungumzo hayo

Nazungumzo yanaendelea

Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania, Bw. Saleh Kusa akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje

Mhe. Waziri na Kaimu Balozi wakiagana huku Katibu Mkuu, Dkt. Aziz Mlima akishuhudia

Picha ya pamoja

No comments: