Gavana wa jimbo la Texas nchini Marekani ameonya kwamba madhara ya yaliyosababishwa na dhoruba na kimbunga Harvey bado yanatarajiwa.Greg Abbott amesema kwamba kata zingine kumi na nne zimeingizwa katika ukanda wa maafa .
Ameongeza kusema kwamba jeshi la taifa hilo ambalo lilipelekwa katika eneo la maafa litaongezwa mara mbili. Nazo fedha za shirikisho la majimbo zinaweza kuzidi dola bilioni moja Iliyotolewa baada ya Kimbunga Katrina kupiga eneo la New Orleans mnamo mwaka 2005.
Mabomba kadhaa ya mafuta na gesi ambayo huliingizia taifa la Marekani robo ya pato la mafuta nchini Marekani kwa sasa yamefungwa.
Mpaka sasa inaarifiwa kuwa watu ishirini wamepoteza maisha kufuatia madhara ya dhoruba hiyo na wengine mia moja na tisini na tano elfu wameorodheshwa kuhitaji msaada wa serikali.
Kimbunga Harvey kwa sasa kimeelekeza nguvu zake upande wa Mashariki kuelekea jimbo jirani la Louisiana.
No comments:
Post a Comment