ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 10, 2017

Polisi Wanne Watiwa Mbaroni kwa Kumjeruhi Mke Wa Mwenyekiti Jijini Mwanza Wakati wakiwa Wamelewa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed Msangi ametoa amri kukamatwa kwa askari polisi wanne wa Kituo Kikuu cha Polisi Nyamagana kutokana na askarii hao kumjeruhi kwa risasi mke wa Mwenyekiti mtaa. 

Kamanda Msangi amesema polisi hao tayari wametiwa mbaroni kwa kumjeruhi kwa risasi mguuni Bi. Editha Ntobi ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Majengo Mapya uliopo katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza.


Msangi amesema polisi hao wanatuhumiwa kufyatua hovyo risasi zaidi ya 10, kuharibu mali za raia lakini pia wanadaiwa kufanya matukio hayo kutokana na kulewa wakati wakiwa kwenye doria kinyume na utaratibu wa kazi yao. 

Bi Editha Ntobi ambaye ni majeruhi wa kupigwa risasi amelazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza kutokana na kuvuja kwa damu nyingi kufutia tukio hilo. 

No comments: