ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 30, 2017

Tundu Lissu aikana tweet kuhusu Diamond, Alikiba

Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni kumpongeza mwanamuziki Alikiba, huku ikiwa na picha ya wanamuziki wanaofanya kazi chini ya lebo wa Wasafi.

Lissu amesema hafahamu chochote kuhusu akaunti hiyo na maoni yaliyotolewa akitaka mwandishi amfafanulie.

“Wananisingizia kaka (mhariri wa Mwananchi), ni wimbo gani wa Alikiba?” akimaanisha haelewi chochote kinachoendelea kuhusu uwepo wa wimbo wa “Seduce Me.”

Amesema akaunti hiyo si yake: “Hiyo akaunti ya Twitter si yangu na nilishasema tangu mwaka jana kaka.”

Jana Agosti 29, akaunti hiyo ilikuwa gumzo kwenye mitandao ikiwa imebeba ujumbe unaosema: “Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme#.

Tweet hiyo iliambatanishwa na picha ya Kundi la Wasafi wakiwa wamevaa mawigi ambayo waliitoa sambamba na wimbo wao wa “Zilipendwa”.

Mashabiki wanaomuunga mkono Alikiba walifurahi wakiamini kiongozi huyo amejiunga na wengine wengi ambao walijitokeza hadharani kumpongeza Alikiba.

Baadhi ya viongozi waliompongeza Alikiba ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla; Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.

1 comment:

Anonymous said...

Kwa nini hao wabunge na mawaziri waliompongeza ALIKIBA hawakutumia fursa hiyo kuwapongeza WASAFI? Ukisikiliza wimbo wa "ZILIPENDWA" kuna mistari mingi ya kihistoria ambayo vijana wengi wanaweza kujifunza, mfano: Wametajwa Iddi Amin, Chama cha TANU, Wabunge wanaofanya GAMBLING, kasi ya serikali ya Magufuli vs Kikwete..etc. Binafsi, nahisi hawa Wanasiasa wamekerwa na yaliyotamkwa kwenye "ZILIPENDWA".
On the other hand, ukitazama Video ya "SEDUCE ME" yupo huyo Mwanadada ambaye anavuta SIGARA na kushika BASTOLA. What morals are we conveying to our youths? Is it okay kwa hawa Wanasiasa kusifia uvutaji sigara (hello..Waziri mdogo wa Afya!) or Bastola? wakati serikali inajitahidi kila siku kupambana na majambazi wanaotumia silaha kama hiyo inayoonyeshwa kwenye "SEDUCE ME" Video? Ni vyema kama mngefanya thorough analysis kabla ya kutoa pongezi. Tusiige mifano mibaya ya Wanamuziki wengi wa mataifa ya magharibi, hususani Marekani. Wengi wapo kwenye lebo kubwa kama ya Alikiba, na licha ya nyimbo nzuri sana wanazozitoa, utakuta video zao nyingi zinaambatana na ushikaji wa silaha, kama Bastola n.k.
Mwisho, nawaomba wadau wenzangu tuache ushabiki usio na tija, badala yake tuangalie madhara ambayo video kama hii inaweza kuleta kwa jamii, zaidi vijana wanaoweza kuwa copycats.