ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 16, 2017

Nyumba ya Zitto iliyopo Kigoma yaungua moto

Nyumba ya Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliyoijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga mjini Kigoma imeungua moto jioni hii.

Nyumba hiyo iko kiwanja kimoja na nyumba yake ya sasa imeteketea yote na chanzo chake hakijafahamika hadi sasa.

Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hatahivyo Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo.

Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na iliyoungua ilikuwa ikitumika kwa dharura.

No comments: