ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 16, 2017

WAANDAMANAJI WACHOMA BENDERA ZA MAREKANI BAADA YA POLISI ALIYEUA MTU KUACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Karibu waandamanaji 1,000 walizingira nyumba ya Meya wa St. Louis Lyda Krewson usiku wa Ijumaa huku wakichoma moto bendera ya Marekani kufuatia mahakama kumuachia huru askari polisi mzungu aliyemuua kwa kumpiga risasi Mmarekani mweusi.
Polisi wa St. Louis wamewakamata watu 13 baada ya mapambano na waandamanaji hao ambapo polisi wanne walijeruhiwa kutokana na uamuzi huo wa Mahakama wenye utata ulioibua hasira za wananchi.
 Polisi mzungu Jason Stockley, aliyekuwa afisa polisi wa St. Louis, Mahakama jana ilimuondolea mashtaka ya mauaji yaliyotokea Ijumaa ya mwaka 2011 yaliyosababisha kifo cha Mmarekani mweusi Anthony Lamar Smith.
Polisi wa kutuliza ghasia wa Marekani wakiwa tayari kukabiliana na waandamanaji huko St Louis
Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba silaha kama inavyoonekana hapa huku wakiwa wamefunika kwa vitamba nyuso zao

No comments: