ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 16, 2017

WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI KITONGOJI CHA ENDEVESI WAJENGEWA SHULE YA MSINGI

Ilikuwa ni siku ya furaha mno kwa wananchi wa jamii ya wafugaji kitongoji cha Endevesi, kata ya Njoro, Wilayani Same. 
Ambapo Septemba 12, 2017 wakati Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule  akipokea majengo ya Shule ya msingi kwa niaba ya serikali. Pamoja Na mradi wa Maji kwa ajili ya wananchi hao wasiopungua 6,000. Shule hiyo yenye madarasa 6, ofisi za walimu, vyoo Na nyumbani za walimu. 
Imejengwa kwa ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith Na Korea Hope Foundation. Jamii hii ya Endevesi walikuwa wakipata Huduma hizi umbali wa km. Zaidi ya 5 Na kupelekea watoto wengi kuwa watoro.
 "Shule tumejengewa, serikali tutahakikisha tunapanga walimu Na shule hii inaanza 2018. Wananchi wakikishe wanaleta watoto shuleni. Nasi tutawachukulia hatua wote watakaokuwa watoro." Aliwashukuru pia kwa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wa Tanzania katika kuhimiza elimu. Miradi hiyo imegharimu zaidi ya Tshs. 800M.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiongea mara  baada ya kupokea majengo yaliyojengwa kwa ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith na Korea Hope Foundation.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wa kumbukumbu.
Mkuu wa wilaya na kiongozi wa Korea Hope Foundation wakinawa mikono katima bomba ambalo ni moja ya mradi waliokabidhiwa.
Makabidhiano yakiendelea.

No comments: