Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), akizungumza na Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, (kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimkabidhi kipeperushi chenye namba ya dharura 114 ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akielekea katika ukumbi wa Mikutano kwa mazungumzo, akiwa ameambatana na mwenyeji wake ambaye ni Afisa habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Neema Mtema (wapili kulia), pamoja na Maafisa wa Jeshi mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimuelezea majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwenyekiti wa Kikao Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru ambaye hayupo pichani, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Viwango wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Bi. Edna Ndumbaro (katikati), akitoa ufafanuzi kwa hatua walizozichukua kuhusiana na vifaa vya Zimamoto, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru (kulia) mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
No comments:
Post a Comment