NA RUKWA YETU BLOG
UONGOZI wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi
9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso
eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.
Katika
kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa
sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote
atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
“Nimekataza
binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu
salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai
maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.
Mh. Zelote
alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza
kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na
kufanikisha zoezi la uokoaji.
Ajali hiyo
ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha
njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa
barabara hiyo.
Lori hiyo mali
ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha
Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia,
kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.
1. Domona
Tenganamba, 41yrs, mfipa mkulima.
2. Emmanuel
Rashid 84yrs, mfipa mkulima, mkazi wa ntemba
3. Restuta
Sunga , 35yrs, mfipa mkazi wa ntemba
4. Salula
Revana 64yrs, mfipa mkazi wa mtapenda isale
5. Ferisia
Tenganamba , miaka 1 – 6/12
6. Prisca
Madeni, 45yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa china
7. Richard
Chikwangara, 24yrs, mfipa, mwalimu mkazi wa kalambanzite
8. Yusta
Somambuto, 36yrs, mfipa, mkulima mkazi wa kizumbi
9. Gilesi
Ramadhan, 24yrs, mfipa, mkulima mkazi wa sumbawanga
10. Odetha
Madirisha 46yrs, mfipa mkulima wa kizumbi
11. Megi
Nalunguli, 52yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
12. Abuu Amani @
mandevu, 37yrs, muha, biashara, mkazi wa liapinda
13. Nyandindi
Batrahamu, 35yrs, mfipa, mkulima, mkazi wa sumbawanga
14. Magdalena
Mbalamwezi, 50yrs, mfipa, mkulima mkazi wa ntuchi
15. Mtoto mchanga
wa wiki mbili, mwanaume ambaye hajapewa jina
Majeruhi wa ajali hiyo ni:-
1. Dismas
Clement, 26yrs, mfipa, mkulima mkazi wa mwinza
2. Sema
Savery 25yrs, mfipa, mkulima mkazi wa wampembe
3. Ally
Haruna, 33yrs, mfipa, mkazi wa namanyere
4. Yusta
Mfundimwa, 50yrs, mkulima mkazi wa izinga
5. Tenesfory
Oscar, 36yrs, mfipa mkazi wa wampembe
6. Amos
Kitambale, 25yrs, mfipa, mkazi wa wampembe
7. Neema
Mwanandenje, 21yrs, mfipa, mkazi wa mlambo
8. Joseph
Sungula, 28yrs, mfipa, mkulima.
9. Majeruhi
mmoja mwanamke ambaye hajafahamika kwa jina yuko icu
Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva alitoroka lakini juduhudi
za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea kufanyika.
Abate wa Pambu Martin Mkolwe Abasia ya Mvimwa akiongoza ibada fupi ya kuwaombea marehemu wa ajali iliyoua watu 15 na kujeruhi 9 iliyofanyika katika kituo cha afya Mvimwa, Wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kaunda Suti ya ugoro) akitoa salamu zake za pole kwa wafiwa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda na kulia kwake ni Abate Pambu Mkolwe wa Abasia ya Mvimwa.
No comments:
Post a Comment