ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 5, 2017

SHIRIKA LA WOTESWA LAWANOA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA.

Na George Binagi-GB Pazzo
Mratibu wa Shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa majumbani WOTESAWA, Cecilia Nyangasi (pichani juu) amesema shirika hilo limejiwekea mikakati ya kuhakikisha kwamba hadi kufikia mwaka 2020 kusiwepo na mtoto chini ya umri wa miaka 18 ambaye ameajiriwa kufanya kazi za nyumbani.

Nyangasi ameyasema hayo hii leo kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari Jijini Mwanza, yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kusaidia kufikisha elimu katika jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na hivyo kuwakosefa fursa mbalimbali ikiwemo kupata elimu.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuwanusuru watoto wafanyakazi wa majumbani na ukatili ikiwemo wa kingono pamoja na kiuchumi ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi bila malipo ama kwa malipo kidogo.

Aidha ametoa rai kwa serikali kuboresha sera, mikakati na sheria zinazomlinda mtoto ili kuondoa mkanganyiko uliopo ambao unashindwa kutambua bayana umri wa mtoto anayepaswa kuajiriwa kwani baadhi hutaja umri wa miaka 14 huku nyingine ikitaja umri wa miaka 18.

Nyangasi amebainisha kwamba mwaka jana shirika la WoteSawa lilifanya utafiti katika Kata nne za Jiji la Mwanza ambazo ni Igogo, Mkuyuni, Butimba na Capriont na kubaini kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na utumikishwaji na ili kupambana na hali hiyo shirika hilo lilianzisha mkakati wa kuwafikia watoto waajiriwa, waajiri wao pamoja na viongozi wa serikali za mitaa na kuwaelimisha.

Nao waandishi wa habari, Moses Mathew kutoka gazeti la Daily News pamoja na Rhoby Magira kutoka Redio Afya wamebainisha kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuandika habari na makala zinazoielimisha jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwatumikisha watoto kupitia ajira za majumbani.

Itakumbuka kwamba mtoto mfanyakazi wa nyumbani analindwa na sheria kadhaa ikiwemo sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, waraka wa mishahara wa mwaka 2013 pamoja na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa upande wa waraka wa mishahara wa mwaka 2013, mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni ingwa waraka huo hautaji mwajiriwa huyo anapaswa asiwe mtoto.

Mkufunzi Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Jijini Mwanza, akisisitiza wanahabari kuungana pamoja katika kuibua na kuandika habari/ makala zenye kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Afisa Habari shirika la WoteSawa akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Moses Mathew kutoka gazeti Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Tazama picha zaidi HAPA

No comments: