ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 8, 2017

BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA BILIONI 340 KUENDELEZA UTALII UKANDA WA KUSINI

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird, wakielekea kusaini Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Katibu Mkuu Wizara ya maliaasili na Utalii( wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya Ujumbe wa Benki ya Dunia walioshiriki tukio la Tanzania na Benki hiyo kutiliana saini mkataba wa mkopo  nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, akitoa neon la shukurani wakati wa kusainiwa kwa Mkataba wa Mkopo Nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola  za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi. Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, huku Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kulia waliosimama-tai nyekundu) akishuhudia, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kulia waliosimama akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakionesha Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, baada ya kusainiwa katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)​

Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 150, sawa na takriban Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.

Mkataba wa mkopo huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi, Bi. Bella Bird.

Bw. James alisema kuwa mkopo huo umelenga kuimarisha miundombinu ya utalii katika ukanda huo wa kusini ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, madaraja pamoja na kuibua fursa nyingi za utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi.

Alisema pia kwamba mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wananchi wanaozunguka maeneo ya utalii kwa kuanzisha miradi itakayo chochea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuendeleza uhifadhi katika maeneo yao.

Aidha, mkopo huo utatumika katika kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda huo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea maeneo hayo badala ya hali ilivyo sasa ambapo watalii wengi wanatembelea vivutio vilivyoko ukanda wa Kaskazini.

Mradi huo utakaotekelezwa kwa kiasi kikubwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania-TANAPA, utainufaisha zaidi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba na Selous.

Alisema kuwa manufaa hayo yatalenga kujengwa viwanja vya ndege, barabara hifadhini, utunzaji wa mazingira utakao uwezesha mto Ruaha Mkuu kutiririsha maji muda wote katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kupitia uwanda wa Usangu.

“Mpango wa kuibua fursa za utalii katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, umelenga kuimarisha usafiri wa anga na nchi kavu ambapo uwanja mkubwa na wa kisasa utajengwa mkoani Iringa pamoja na kuboresha barabara inayotoka Iringa hadi Msembe yenye urefu wa kilometa 105” alisema Bw. James

Aisema kuwa hatua hiyo inatarajia kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi na kupunguza gharama za usafiri kutoka katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Kilimanjaro hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Bw. Doto James aliishukuru Benki ya Dunia kwa mkopo huo utakao changia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi wake kupitia sekta ya utalii.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali, Gaudence Milanzi alisema kuwa mradi huo, utahusisha ujenzi wa viwanja 15 vya ndege, ujenzi wa kilometa 982 za barabara kwenye hifadhi, kununua mitambo ya kukarabati barabara, kuimarisha reli ya TAZARA ili kuwawezesha watalii kufika kwenye Pori la Akiba la Selous.

Aidha, alisema kuwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi watapatiwa mafunzo ya namna ya kuongoza watalii, kutoa huduma kwenye hoteli na kuwajengea uwezo wa kutengeneza bidhaa zinazohusiana na utalii ili wajiongezee kipato.

Meja Jenerali Milanzi alisema kuwa wanategemea mradi huo utaongeza idadi ya watalii kutoka milioni moja hivi sasa hadi kufikia zaidi ya watalii milioni 2 ifikapo mwaka 2020.

Akizunguza wakati wa tukio hilo, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, hapa nchini Bi. Bella Bird alisema kuwa mkopo huo ulioridhiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Jijini Washington DC Septemba 28, 2017, umelenga kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta hiyo ya utalii na kupunguzia umasikini wananchi wake.

“Utalii na uhifadhi vinakwenda pamoja na kwamba vitu hivyo viwili vitaisaidia nchi kukua kiuchumi na kukuza ajira ya watu wake kwa kiwango kikubwa hivyo kuondokana na umasikini ikichagizwa pia na kilimo” alisisitiza Bi. Bella Bird.

Alisema sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya watu na wanyama, ujangili, na ndiyo maana Benki ya Dunia imeamua kuisaidia Serikali na taasisi zinazojihusha na kudhibiti changamoto hiyo kwa kuzijengea uwezo wa kukabiliana nazo.

Bi. Bird alisema kuwa mradi huo utakuja na suluhisho la changamoto ya wananchi kuwa sehemu ya uhifadhi kwa kuwapa miradi ya maendeleo itakayokuwa mbadala wa shughuli walizokuwa wakifanya kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuanzisha utalii wa kiutamaduni, kilimo ili waendeleze maisha yao.

No comments: