Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira
Mgalu, (kulia) akizungumza jambo mbele ya viongozi wa Tanesco mkoa
wa Temeke na wa serikali ya Mtaa, alipotembelea miradi ya umeme huko
Chamazi, Dovya, Mbagala jijini Dar es Salaam, leo Jumapili Novemba 5,
2017.
NA
MWANDISHI WETU
NAIBU
Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu leo Jumapili Novemba 5, 2017 amefanya ziara
ya kutembelea miradi 7 ya umeme inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania,
(TANESCO), huko Chamazi-Dovya kwa Mzala 1-3, Mbande kwa Masister na Chamazi
Vigoa, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Waziri amefuatana na Kaimu Mkurugenzi, TANESCO, Mhandisi Dkt.
Tito Mwinuka na viongozi wengine wa Shirika hilo.
Kwa
mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, miradi hiyo saba
ni pamoja na ule wa Chamazi Dovya ambao unajumuisha miradi mitatu, (3), Mbande
kwa Masister, Miradio 4 na hivyo kufanya jumla ya miradi saba lengo likiwa ni
kuwapatia umeme Wananchi wote wa Chamanzi Dovya ambao hawajapata
umeme.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka(wapili kushoto), Meneja Mwandamizi wa
TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mgaya,
(wakwanza kushoto) wakimsikiliza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke,
Mhandisi Jahulula, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi
hiyo.
Naibu waziri Mgalu akiangalia ripoti
ya utekelezaji wa miradi hiyo, iliyokuwa ikisomwa na Meneja wa TANESCO
Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula Maendeleo.
No comments:
Post a Comment