MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara kikosi cha Yanga, kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba huku wakitamba kuwafunga Mbao FC wanayocheza nao kesho Jumapili, lakini kinachofurahisha na kuwashangaza wengi ni ulinzi mkali wanaoufanya.
Kikosi cha Yanga, kilitua jijini Mwanza jana Ijumaa kwa usafiri wa ndege ambapo tangu wamefika, kumekuwa na ulinzi mkali, kuanzia hotelini walipofikia, mazoezi na hata katika Uwanja wa CCM Kirumba ambako kutachezwa mchezo huo.
Benchi la ufundi lililo chini ya kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa wamesema. maandalizi waliyoyafanya yatatosha kuwaangamiza Mbao na wanapata matumaini zaidi, uwepo wa straika Mrundi Amiss Tambwe..
"Haya ni mazoezi ya mwisho, vijana wameelewa kwa hiyo tunasibiri watekeleze tulichowafundisha tu, kurejea kwa Tambwe ni tumani jingine kwa sababu ni mchezaji anayepambana katika upatikanaji mabao"amesema Nsajigwa.
Kocha huyo ameongeza kuwa wanaingia uwanjani kwa tahadhari kubwa wakiamini wapinzani wao wana
uwezo kwenye mbinu, hivyo wamejiandaa.
MAZOEZI YA LEO CCM KIRUMBA
Katika mazoezi yao ya asubuhi waliyofanya Uwanja wa CCM Kirumba, makomandoo wa Yanga
walionekana hawataki mchezo kwenye suala la ulinzi, walizunguka huku na kule kuhakikisha hakuna mtu anavamia na kufanya vikao vya hapa na pale.
Mmoja wa mashabiki ambaye alikuwa makini kuongoza wenzake, Charles Kabunda amesema mechi
ya kesho hawataki mzaha, badala yake wanakufa na pointi tatu: ”Hatutaki masihala hapa, lazima kila mmoja wetu atimize wajibu wake, kesho hatoki mtu hapa."
mwanaspoti
No comments:
Post a Comment