Timu ya Vijimambo Blog kwanza kabisa tunapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutujalia leo kuona mwaka mpya 2018 na Blog yako inapenda kuwatakia wadau wote wa Blog hii pendwa kheri ya mwaka 2018, mwaka uwe na mafanikio kwa wadau wote Duniani.
Timu ya Vijimambo Blog inapenda kuchukua nafasi hii pia kuwashukuru wadau wake wote kwa ushirikiano wa karibu mnaouonyesha kwenye Blog yenu na jambo linalotutia moyo na kuendelea kuwa daraja la habari, burudani na kiunganishi cha Diaspora na nyumbani.
Timu ya Vijimambo Blog inatoa shukurani kwa Blog zingine kwa ushirikiano wa karibu unaondelea katika tasnia hii ya habari ulimwenguni bila nyinyi Vijimambo tusingefikia hapa tulipo.
Timu ya Vijimambo inapenda kushukuru IKULU, Wizara zote ikiwemo Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Wizara ya mambo ya ndani, MAELEZO, Ubalozi wa Marekani Tanzania, Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC, Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York kwa kuitambua na kuiamini Vijimambo Blog kama chombo kinachoweza kuwafikishia habari wadau wote wanaokizunguka kwa wakati muafaka na kwa muda kunapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo..
Timu ya Vijimambo Blog inapenda kutoa shukurani za pekee kwa Jumuiya zote za Watanzania Diaspora kwa ushirikiano wa karibu sana unaotolewa na Jumuiya hizo kwa Blog yao pendwa.
Timu ya Vijimambo inapenda pia kuchukua nafasi hii kipekee zaidi kuishukuru DICOTA kwa kukubali kuitumia Vijimambo Blog na kuiamini kama chombo kinachoweza kufikisha habari zao kwa uhakika na haraka kwenye jamii ya Diaspora na kuwa kiunganishi cha Diaspora na nyumbani.
Timu ya Vijimambo Blog inapenda kuwashukuru Umoja wa Diaspora Duniani (TDC Global) kwa ushirikiano wa karibu inaopata kutoka kwa viongozi wao.
Timu ya Vijimambo Blog inawatakiwa wadau wote amani na upendo na kuitanguliza TANZANIA KWANZA na asante sana kwa ushirikiano wenu, Mwenyezi Mungu awajalie baraka tele katika mwaka huu wa 2018. na kauli mbiu yetu ni KUWA MZALENDO, IPENDE NCHI YAKO, TANZANIA KWANZA..
No comments:
Post a Comment