Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi Mara baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo 2 Februari 2018.Picha Zote Na Mathias Canal
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab R. Telick akitoa taarifa ya sekta ya madini katika Mkoa huo mbele ya Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka, leo 2 Februari 2018.
Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na watumishi mbalimbali katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo 2 Februari 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab R. Telick akitoa taarifa ya sekta ya madini katika Mkoa huo mbele ya Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka, leo 2 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Shinyanga
Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab R. Telack za kukabiliana na migogoro mbalimbali inayojitokeza jambo ambalo linarahisisha na kuboresha utendaji wa Wizara ya madini nchini.
Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo leo 2 Februari 2018 wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi Mara baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Shinyanga.
Katika ziara hiyo iliyoanza Leo 2 Februari 2018 na kumalizika kesho 3 Februari 2018 katika Mkoa wa Shinyanga Naibu Waziri huyo wa wizara ya madini atatembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Mwazimba na Wachimbaji wadogo wa kikundi cha Kasi Mpya.
Mhe Biteko amemweleza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuongeza msisitizo zaidi katika usimamizi madhubuti wa sheria, Kanuni na taratibu za nchi pamoja na kuwa na majukumu ya sekta zote lakini sekta ya madini aongeze juhudi pia ili kuinua mpango wa Wizara ya madini kuongeza nguvu katika mchango kwenye pato la Taifa kufikia asilimia 10% kutoka asilimia 4% ya sasa.
Naibu Waziri huyo amesema serikali ngazi ya wilaya na Mkoa ni vema wakaendelea kuwalea wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa katika utekelezaji wa sheria ya madini na kanuni zake.
Aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa na watendaji wote wa sekta ya madini hawapaswi kuogopa migogoro katika sekta hiyo kwani ili kuwasaidia wachimbaji wadogo ni lazima kukabiliana na migogoro mbalimbali inayojitokeza baina ya wachimbaji wenyewe na wawekezaji sambamba na sintofahamu baina yao na baadhi ya watendaji wa serikali.
Aidha, amekitaka chama cha wachimbaji wadogo nchini kuisaidia serikali kufichua uovu unaofanywa na baadhi ya wachimbaji Wasio waaminifu ikiwa ni pamoja na utoroshwaji wa madini mbalimbali jambo ambalo ni kuwaibia watanzania na kinyume na Sheria ya madini sambamba na usafirishaji wa madini.
Mhe Biteko aliongeza kuwa wachimbaji wadogo na wakubwa kote nchini wanapaswa kujibainisha katika ulipaji kodi kwani kufanya hivyo kutaimairisha utendaji wa Wizara katika mchango wa pato la Taifa ikiwa ni pamoja na serikali kuwatambua na kuongeza ufanisi wa kuwahudumia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa alimweleza Mhe. Biteko serikali ya Mkoa wa Shinyanga imejipanga kusimamia vema sekta hiyo kwani ni nguzo kubwa ya uchumia wa Mkoa huo na akaiomba Wizara ya madini kuendeleza ushirikiano na ofisi yake ili kuongeza tija katika usimamizi wa sekta ya madini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake