NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC )Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa Iringa itamshughulikia mtendaji yeyote wa Serikali atakayeonyesha dalili ya kukwamisha juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa mwiki alipokuwa akiongea na wananchma wa CCM Manispaa ya Iringa katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM ,alisema Mtu yeyote ndani ya serikali ya mkoa wa Iringa atakayeonyesha dalili za kuhujumu au kwa makusudi, serikali ya chama cha mapinduzi haita muacha na lazima itamshughulikia.
“Nasema hatuta kubali kuona mtu yeyote atakaye onyesha kukwamisha juhudi wakati rais na mwenyekiti wetu wa Taifa tutapambana nae,Rais amejitoa kwa wananchi wake alafu mtu atokee tu na kuvuruga utaratibu lazima haiwezekani na tutapambana nae”alisema MNEC
Alisema Wakuu wa Wilaya wanapaswa kuwaambia viongozi wao wa serikali kuwa kofia na nguo za kijani ndiyo wanaosimama kwenye majukwaa kuwatete wao,hivyo si haki CCM tubebe lawama kwa ajili ya hao watendaji wazembe wenye nia ovu kwa serikali ya kukwamisha maendeleo ili wengine wapande jukwaani wakitukane chama Tawala.
hivyo aliwataka viongozi wa chama hicho kujua majukumu yao ya kuhakikisha CCM inasimammia Serikali na si wengine wanasimama kutetea uozo wa watendaji hao ambao nia yako ni mbaya lakini kama watendaji wangejua thamani ya CCM basi ingekuwa vigumu kuwepo mtendaji wa serikali ambae ni mpinzani.
Abri ( ASAS ) aliongeza kuwa Ilani inataka yaale mambo yaliyaidiwa kwa wananchi yanatekelezwa kwakuwa wakati wa kuomba kura ni wanaCCM ndiyo waliosimama kuomba kura na si taasisi za serikali au Mkurugenzi wa Halmashauri,hivyo hatuna budi kuhakikisha Ciongozi wa CCM wanafuatilia utekelezaji wa Ilani kwani hata pale yasipotekelezwa wananchi halaumu chama tawala na si watendaji wa serikali.
“Sisi viongozi wa mkoa hapa wa CCM ndiyo wawakilishi wa mwenyekiti wetu na madhumuni ya ccm ni kuisimamia serikali ,haiwezekani CCM tunatukanwa ovyo kwa ajili ya wazembe,wakati serikali inasema hakuna michango mashuleni lakini mwalimu mwenye itikadi ya kipinzani anafukuza mwanafunzi eti bila michango hakuna kuingia”.
Alisema MNEC “Haiwezekani Rais afanye kila juhudi alafu watokee watu wengine wajinga tu hivi waanze kukamisha ,sisi hapa wajumbe wa Halmashauri kuu,mwenyeviti na na viongozi wengine ndani ya chama kazi yetu nini, yaani rais atoke ikulu aje Iringa kushughulikia watu hao ”.
Aliongeza kwakusema “haiwezekani wananchi maskini watekeseke kwa ajili ya wapuuzi puuzi wajanja ,rais kila siku anapiga kelele muwe kwenyenupande wa wanyonge au upande wa maskini ,lakini kuna watu ambao kazi yao ni kikwamisha juhudi na kubeza kazi inayofanya Rais Magufuli tunasema hatuta kubali “
Au mtu yeyote wa serikali atakaye taka kukwamisha juhudi za Rais na Mwenyekiti wetu wa Taifa lazima tutamshughulikia na wanaCCM wawashughulikie kwa sababu wanaotukwanwa ni chama cha mapinduzi na ni kwa ajili ya uzembe wa watendaji wa serikali wasiokipenda chama
“Kwa sababu CCM ndiyo chama kilichopo madarakani na hata kwenye kuomba kura wao hawakuwepo lakini Mkurugenzi au mwandisi amepewa fedha ya kutengeneza barabara alafu akala hela nawauliza lawama itaenda kwa nani kwa kawaida itaenda kwa chama tawala ambacho ndiyo CCM basi na sisi tusikubali”alisema,
Pia aliwataka wanaCCM wa mkoa wa Iringa kuwapuuza wale watendaji wa serikali wanaosema hali ngumu kwani hao ndiyo watumishi waliozoea kula rushwa,mafisadi na watendaji wasiokuwa na maadili ya kazi.
“Alafu wapuuzeni wale na watumishi wa serikali na viongozi wanaokasikiri na kulalamika kuwa hali ngumu,vyuma vimaekaza sasa mimi namuuliza mshahala wako huupati anaupata katika tarehe zilezile na je mshahara umepunguzwa hapana ni uleule sasa ugumu unatoka wapi ,nikagundua kuwa hao ndiyo wanaotupa tabu serikalini”alisema Abri .
Aidha amewashukuru wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Iringa wa CCM kwa kuwafuta machozi wanaManispaa ya Iringa ,hawa wamekuwa mstali wa mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika Manispaa hii lakini si kama wahawajali wa mufindi,kilolo wa Iringa Vijijini ni kutokana majimbo hao kuwa na wabunge wa ccm lakini Manispaa ni yatima.
“Katika miaka miwili na nusu Manispaa ya Iringa imeonza zahama kubwa kwani hakukuwa na lolote lililofanyika katika jimbo hili zaidi ya maneno tu”alisema
Alisema anashangazwa na Ofisi ya Meya ambayo ni ya serikali kugeuzwa ndiyo ofisi ya kutolea matamko ya chama chao “kila mara inawaita waandishi wa habari kutoa matamko ya kisiasa ya chama chao na si kuwaita kuwaeleza wamefanya nini lakini katika Manispaa ya Iringa lakini hutaona CCM inatumis majengo ya Serikali kutolea matamako kwa sababu CCM inaofisi zao”.
Pia MNEC aliwata WanaCCM wa Manispaa ya Iringa kuhakikisha hawafanyi makosa kama waliofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 inatakiwa waseme sasa basi.
“unajua kweli wanasiasa tunacheza siasa lakini tusicheze kwenye maisha ya watu sanjali na hali za watu ,tusiweke utani wa siasa kwenye maisha ya watu kwani siasa si kama ushabiki wa mpira,tunajenga maisha ya watu ,manispaa yetu inakuwa kila kukicha kwa kuwa watuwanaongezeka”alisema MNEC .
Awali akimkaribisha Mgeni RAsmi ambaye ni MNEC wa Iringa ,Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magalla aliwata aliwata watendaji wa serikali na taasisi zake kuwa watekerezaji wa sera na maamuzi ya chama tawala kwani ndiyo chama kilichochaguliwa na wananchi.
Kwa hiyo asitokee mtendaji yeyote wa serikali au kiongozi anayetaka kukwamisha sera na maamuzi ya CCM bali wawe mstali wa mbele katika kutatua kero za watu na si wao kuwa sehemu ya kero kwa wananchi wao wanaowategemea .
Magalla alisema watendaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanangaile na shida za wananchi kwani hivi sasa kumekuwa viongozi wa serikali ndiyo wamekuwa kero kwa wananchi kwa kuwasumbuasumbua mara kwa mara bila hata kuwapa elimu kwanza wananchi kabla ya kuwavunjia au kukamata vifaa vyao aambavyo ndiyo vinawaingizia kipato.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake