ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 17, 2018

Mtulia: Nitakubaliana na Matokeo Yoyote

Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulid Mtulia amefunguka na kudai atakubaliana na matokeo yoyote yatakayo tangazwa jioni ya leo na Tume ya Uchaguzi Taifa (NEC) pindi zoezi la kuhesabu kura litakapomalizika.

Mtulia ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anafanya mahojiano ya mubashara kutokea katika kituo alichopigia kura cha Friends Corner, Kata ya Ndugumbi na kusema zoezi hilo linakwenda salama mpaka hivi sasa na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili washiriki katika zoezi hilo ambalo ni haki yao ya kimsingi.

"Chama changu sio cha ulalamishi na hata kama kikiona hakikutendewa haki huwa kinafuata njia za kisheria kwa kufungua kesi Mahakamani kulalamikia matokeo lakini tutayakubali matokeo yeyote yatakayo kuja jioni", amesema Mtulia.

Jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini leo yameingia katika zoezi la kupiga kura za kuchagua wabunge watakaoweza kuwakilisha shida za wananchi wa majimbo hayo Bungeni.

No comments: