Saturday, February 3, 2018

TAARIFA KWA UMMA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANACHAMA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII


Bi. Sarah Kibonde Msika, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), akiongea na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii alipokua akiongea kuhusu zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii alipokua akiongea kuhusu zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Bw. Francis Saliboko, Meneja Data - Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Bi. Sarah Kibonde Msika, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari. Kulia ni Bw. Emili Mkaki, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).


Bi. Sarah Kibonde Msika, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji, Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi yaJamii.

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Description: C:\Documents and Settings\Nida\My Documents\My Pictures\logo.png

TARATIBU ZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANACHAMA WA MIFUKO YA JAMII NCHINI
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inawajulisha wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini watakaosajiliwa kupata Vitambulisho vya Taifa kuzingatia yafuatayo:-

  • Watakaosajiliwa ni watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, Raia wa Tanzania na wageni wanaoishi kihalali nchini na awe mwanachama wa mfumo wa Hifadhi ya Jamii.
  • Fomu za kujisaji zinapatikana kwa mwajiri wako, Ofisi ya Serikali ya Mtaa unakoishi au Ofisi ya NIDA na hakikisha umejaza fomu hiyo vipengele vyote kwa kalamu nyeusi na kuweka viambatisho muhimu vitakavyokutambulisha Umri, Makazi na Uraia. Vielelezo hivyo ni Cheti cha Kuzaliwa, Pasi ya kusafiria (Passport), vyeti vya shule ( Msingi, Sekondari),  Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na Kitambulisho cha Kupigia Kura na kitambulisho cha kazi.  Kuwa na Viambatisho vingi zaidi ni kutambulika kwa haraka zaidi. (Viambatisho vyote ulivyonavyo vitoe nakala (photocopy) na kuambatisha na fomu yako ya maombi kwa ajili ya hatua ya kupigwa picha, kuchukuliwa alama za vidole)
  • Kwa wageni wawe na Passport ya nchi alikotoka, kibali cha kuishi nchini na kibali cha kufanya kazi vinavyotolewa na Serikali.
  • Hakikisha fomu yako kipengele namba 59 umesaini wewe, No. 60 -  Kimejazwa na Mwenyekiti au mtendaji wa Mtaa unaoishi na Kipengele Na.70 – kimejazwa na Mwajiri.
  • Baada ya kukamilisha hatua za awali za Usajili kutakuwa na hatua ya Uhakiki wa Taarifa na mapingamizi.

Uchukuaji alama za Vidole, Picha na Saini ya Kielektroniki utafanyika kuanzia tarehe 05 /02 hadi 28/02/2018 kwenye vituo vifuatavyo :-

    • Ilala – Ofisi za PSPF, Jengo la Golden Jubilee, Mtaa wa Ohio
    • Kinondoni – Ofisi za LAPF Jengo la Millennium Tower, Kijitonyama
    • Temeke – Ofisi za PPF, Tazara
    • Ubungo – Ofisi za GEPF Ubungo Plaza
    • Kigamboni – Ofisi za NSSF, Darajani
Unapofika kwenye kituo unashauriwa kwa ubora wa picha usivae nguo nyeupe, bluu, pinki au nguo yoyote inayoshabihiana na nyeupe, kupata hina kwenye vidole, kuvaa kofia au T-shirts zenye maandishi/ michezo au kuvaa kofia.


Vitambulisho vya Taifa kwa Malendeleo ya Taifa

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII
Description: C:\Users\user\AppData\Local\Temp\SSRA Logo.jpg
TAARIFA KWA UMMA
ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANACHAMA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Ili  kuboresha taarifa za wanachama wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini,Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), wanaendelea na  zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa kwa wanachama wa Mifuko yote ya Hifadhi za Jamii nchini

Awamu ya pili ya zoezi hili imepangwakuanza tarehe 05/02/2018 hadi tarehe 28/02/2018mkoani Dar es Salaam ambapo wataandikisha wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao hawajawahi kusajiliwa na NIDA.Vituo vitakavyo tumika katika uandikishaji ni:-
    • Ilala – Ofisi za PSPF, Jengo la Golden Jubilee, Mtaa wa Ohio
    • Kinondoni – Ofisi za LAPF Jengo la Millennium Tower, Kijitonyama
    • Temeke – Ofisi za PPF, TAZARA
    • Ubungo – Ofisi za NSSF Ubungo Plaza
    • Kigamboni – Ofisi za NSSF, Darajani

Mwanachama atakayehitaji kusajiliwa atatakiwa kuwa na vielelezo vifuatavyo: Cheti cha kuzaliwa, Pasi ya Kusafiria, Vyeti vya Shule (Msingi na Sekondari), Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Kupigia Kura na Kitambulisho cha Kazi.
Pia atatakiwa kuzingatia kanuni na taratibu za Usajili kama zitakavyoelekezwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia tovuti ya NIDA ambayo ni www.nida.go.tz.

Kwa maelezo au ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii(SSRA) kupitia namba 0656 631253na 0715 557676 au barua pepe info@ssra.go.tz.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam.
02/02/2018

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake