ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 15, 2018

Afande Sele atambulishwa rasmi CCM

Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kupitia ACT-Wazalendo mwaka 2015, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, leo Alhamisi Machi 15, 2018 ametambulishwa rasmi kama mwanachama wa CCM mbele ya Rais John Magufuli.
Baada ya utambulisho huo uliofanyika baada ya Sele ambaye pia ni mwanamuziki wa kizazi kipya, kutumbuiza moja ya nyimbo zake zilizotamba mwanzoni mwa miaka ya 2000, alivalishwa sare za chama hicho tawala na kupeana mkono na Rais Magufuli.
Afande Sele amekaribishwa leo ndani ya CCM katika hafla fupi ya uzinduzi wa kiwanda cha sigara cha Philip Moris Tanzania kilichopo mkoani Morogoro.
Hata hivyo, msanii huyo alikihama ACT takriban mwaka mmoja uliopita na kujiunga na CCM.

No comments: