Diwani wa Kata ya Ifunda Bw. Elicus Chumila Ngwetta akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea eneo la Ifunda na kujionea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichohifadhiwa vizuri. Uhifadhi wa vyanzo vya maji ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Kangi Lugola akifafanua jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Kamati ya Bunge mwishoni mwa wiki ilipata fursa ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akiwaonyesha waheshimiwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mifugo kunywa maji katika eneo la Ifunda ikiwa ni jitahada za Mkoa huo kuhifadhi vyanzo vya maji.
Kamati ya Kudumu ya Bunge Biashara na Mazingira mwishoni mwa wiki imetembea chanzo cha Maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoani Iringa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa jitihada zao za kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kunyweshea mifugo ili kuendelea kulinda vyanzo vya maji na kuwataka kuondoa miti iliyopo pembezoni mwa chanzo hicho ambayo inanyonya maji kwa wingi.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola amezitaka Halmashauri na Wilaya zote nchini kupanda miti kwa wingi ambayo ni rafiki kwa mazingira. “Endapo tutapanda miti kwa wingi, tutaendelea kuwa na mvua za kutosha na kila Halmshauri zinatakiwa kuwa na Sheria ndogo ndogo za Mazingira”
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amewataka waheshiwa wabunge kuwa mstari wa mbele kuhimiza kilimo cha umwagiliaji kwa kutimia ‘matone’ ili kupunguza matumizi ya maji katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment