ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 22, 2018

Ajali yaua watatu, yajeruhi wawili

By Julieth Ngarabali, Mwananchi jngarabali@mwananchi.co.tz

Chalinze. Watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuelekea Dodoma kupinduka.

Ajali hiyo imetokea jana jioni Jumatatu Mei 21, 2018 eneo la Mtelela Barabara ya Msolwa Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumza na MCL Digital, mganga wa zamu wa kituo cha afya Msoga, Dk Nelson Luoga amesema wamepokea majeruhi wawili; Priscus Chuwa na Godfrey Kilolo ambao wote ni watumishi wa kituo cha uwekezaji (TIC).

Amesema waliwapa huduma ya kwanza lakini baada ya hali zao kubadilika waliwapa rufaa kwenda Hospitali ya Tumbi Kibaha na baada ya vipimo zaidi usiku wa kuamkia leo walipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Amesema waliofariki ni watumishi wa umma, kubainisha kuwa katika kituo hicho hawakupokea miili ya watu hao, zaidi ya majeruhi ambao tayari wamehamishiwa Muhimbili.

No comments: