Advertisements

Monday, July 23, 2018

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KITUO CHA AFYA CHA NANYALA WILAYANI MBOZI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amefungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh.Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Muonekano wa jengo la  kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi
 Jiwe la Msingi lililowekwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia mapema leo mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi  mapema leo mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wakazi wa Wilaya ya Mbozi kwa kujiunga kwa wingi katika huduma ya Bima ya Afya ambapo zaidi ya asilimia 77% ya wananchi wa mkoa wa Songwe wamejiunga na huduma hiyo ya bima.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akihutubia wakazi wa kata ya Iyula kwenye viwanja vya mikutano vya Iyula B ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 mkoani Songwe.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa wananchi wa wilaya ya Mbozi kujikinga na ukimwi ambapo aliwaambia kila mwananchi anawajibu wa kujilinda mwenyewe.

Aidha Makamu wa Rais amepongeza wananchi kwa kuitikia wito wa chanjo ambapo zaidi ya ailimia 80% ya chanjo imechanjwa kwa mama na mtot0.

Mapema leo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichogharimu shilingi milioni 820 ambapo wakazi zaidi ya elfu kumi kutoka vijiji vitano katika kata ya Nanyala watapata hudumua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Iyula ambao utawasaidia zaidi ya wananchi 46,000.

Makamu wa Rais amewaeleza wananchi wa kata ya Iyula kuwa Mheshimiwa Rais ametoa uzito mkubwa katika maji hivyo nguvu kubwa imewekwa katika kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa wananchi.

“Tuendelee kuunda jumuiya za maji ili tutunze vyanzo vya maji na miundo mbinu ya maji.” Alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amewasihi wananchi wa mbovu kutunza mazingira kwa kupanda miti na kulinda vyanzo vya maji.

Akizungumzia masuala ya uwekezaji wa viwanda katika wilaya ya Mbozi, Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha miundo mbinu ya barabara, umeme na maji ili kuvutia wawekezaji zaidi wilayani hapo.

No comments: