Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili leo tarehe 15 Agosti 2018 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek, Namibia ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018.
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mawaziri wa Serikali ya Namibia waliowasili kumpokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek, Namibia. wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Christine !!Hoebes na wa kwanza kushoto ni Waziri wa Elimu ya juu, Mafunzo na Ubunifu, Mhe. Dkt Itah Kandjii-Murangi.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Ali Khamis Juma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Namibia mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Mhe. Sylivester Ambokile mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais , Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana Naibu Mwanasheria Mkuu, Dkt. Evaristo Longopa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek, Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Theresia Samaria mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Edwin Mhede mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataiafa wa Hosea wa Kutako mjini Windhoek, Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Innocent Shiyo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agness Kayola mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Zulekha Fundi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek,Namibia.
No comments:
Post a Comment