ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 17, 2018

MADAKTARI KUTOKA MAREKANI WAFANYA MAKUBWA KONDOA

Baada ya kumaliza ziara ya huduma za afya Zanzibar. Leo ni siku ya kwanza katika hospital ya Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma, Tanzania. 
Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana.HEAD, INC
Madaktari kutoka Marekani waliopelekwa nchini Tanzania na Head, Inc leo wamefanya shughuli zao za kitabibu katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma na umati wa watu ulijitokeza katika kupata huduma ya afya isiyokua na malipo kutoka kwa madaktari hao ambao pia walikwenda na madawa kibao kwa ajili hiyo. Madaktari kutoka Marekani wapo nchini Tanzania tangia wiki iliyopita na walianzia kutoa huduma hiyo Zanzibar.
Wagonjwa mbalimbali waliofika katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa katika kupata huduma ya afya bure kutoka kwa madaktari kutoka Marekani.
Madaktari kutoka Marekani walipolekwa nchini Tanzania na Head, Inc taasisi isiyo ya kiserilali inayoendeshwa na waTanzania waishio DMV wakitoa huduma ya afya bure Wilayani Kondoa.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

1 comment:

Anonymous said...

Hongera sana Head Inc. Ninyi ni mfano wa kuigwa.