KAIMU Mtendaji Mkuu wa FETA kulia akiteta jambo na uongozi wa wilaya ya
Pangani kushoto anayemsikiliza ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu
Issa na kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakati walipofika ofisini
kwake
KAIMU
Mtendaji Mkuu wa FETA akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa
Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa
Aweso kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo FETA kushoto ni Mkuu
wa wilaya
ya Pangani Zainabu Abdallah na anayefuatia ni Afisaa Tawala wa wilaya ya
Pangani Gibson
Siku chache baada ya kikao na Waziri wa Uvuvi na Ufugaji; Mh. Luhaga
Mpina na Uongozi wa wilaya ya Pangani chini ya Zainab Abdallah na
Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso wamefanya ufatiliaji wa haraka
sana kupelekea ufanikishaji wa upatikanaji wa Mashine Engine za boti za
kuvua mazao ya baharini.
Hatua hiyo ni baada ya kufanya ziara kwenye Chuo cha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency - FETA); makao makuu wilayani Bagamoyo (Mbegani) walipokwenda kufatilia, na kupata uhakika wa Engine zenye thamani ya takribani sh.Milioni 80 kwa ajili ya wana Pangani wanaojihusisha na sekta hii ikiwa ni matokeo chanya ya haraka sana. Tunamshkuru Katibu Mkuu (Uvuvi) Dr Rashid Tamatama kwa kufanikisha hatua hii muhimu.
Akizungumza baada ya hatua hiyo muhimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa alisema hayo ni mapinduzi makubwa ambapo engine hizi zinaenda kuwasaidia vijana wengi na kuimarisha zaidi sekta hii.
Alisema pia ni kujifunza na kujionea namna chuo kinavyo endeshwa ikiwa ni sehemu ya kujiandaa ufanikishaji wa mafunzo yanayotolewa hapo kutolewa Chuo Cha KIM kilichopo Pangani baada ya kupata suluhu ya sintofahamu ya muda mrefu iliopo.
Hata hivyo viongozi wa wilaya ya Pangani walitoa shukrani za dhati kwa Wizara ya Uvuvi kwa namna walivyo na utayari mkubwa wa kushughulika na changamoto za watanzania ikiongozwa na Waziri Mpina na Naibu Waziri Ulega ambae wiki ijayo atafika Pangani kuweka sawa mengine mengi kuelekea uimarishaji wa sekta hii tegemezi No.1 la mapato ,uchumi na ajira Pangani.
#Panganiyetu
#SektakwaSekta
No comments:
Post a Comment