|
Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
|
19 Septemba 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea wa
Kimarekani la Peace Corps lawaapisha Wafanyakazi wa Kujitolea 59 wa sekta ya
Elimu
Korogwe, TANZANIA. Tarehe 19 Septemba
2018, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson aliongoza hafla ya
kuapishwa kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 59
watakaohudumu nchini Tanzania kwa miaka miwili katika sekta ya Elimu. Wafanyakazi
hawa watapangiwa kufanyakazi katika wilaya 35 nchini kote Tanzania.
Dk. Patterson aliongoza kiapo rasmi cha wafanyakazi hao
wapya wa kujitolea mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe.William Tate Olenasha. Hafla
hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wa serikali, wafanyakazi wa kujitolea wa
zamani wa Peace Corps, wawakilishi wa taasisi wabia na wanafamilia wa familia
za Kitanzania ambazo wafanyakazi hawa wa kujitolewa waliishi nazo.
Kaimu
Balozi Patterson aliwaeleza wafanyakazi wapya wa kujitolea kuwa: "Wakati
ambapo ninyi mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kukutana na kufanya kazi na
wafanyakazi wenzenu na majirani zenu wa Kitanzania, ni dhahiri kwamba katika
mawazo yao mtaendelea kuwa wawakilishi wa watu wa Marekani na ubia wa muda
mrefu kati ya Wamarekani na Watanzania."
Peace Corps
ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka
1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya
7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa zaidi ya miaka 50, Peace Corps
imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na
kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina
dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu
yafuatayo:
- Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani
watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi
itakayohitaji wafanyakazi hao:
- Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu
katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;
- Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na
watu wake.
Zaidi ya
wafanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps 3000 wamehudumu nchini Tanzania toka
mwaka 1961. Peace Corps hutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wenye
utaalamu katika nyanja mbalimbali ambao hupangiwa kufanyakazi katika jamii
wakifundisha katika shule za sekondari (hisabati, sayansi na Kiingereza),
wakitoa elimu ya afya na utunzaji wa mazingira.
Kwa taarifa zaidi,
tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa
simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov
No comments:
Post a Comment