Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na watumishi wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Pia Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kuwataka baadhi ya viongozi wa wizara hiyo kuacha tabia ya kuwanyanyasa watumishi wao. Lugola alikutana na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Veta, jijini Dodoma, leo jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu alipokua anawasili katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi na watumishi
mbalimbali wa wizara yake wafanye kazi kwa kushirikiana na kuacha tabia ya kunyanyasana
wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.
Lugola pia amesema kila mtumishi wa wizara yake ana umuhimu mkubwa kwa kufanikisha
mafanikio ya wizara hiyo kwakuwa watumishi hao wanafanya kazi kwa kutegemeana.
Akizungumza na watumishi wa makao makuu wa wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa
Chuo cha Veta, jijini Dodoma jana, Lugola alisema kikao hicho alikiitisha kwa lengo la kujuana
na watumishi hao pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi.
“Mambo muhimu ambayo yatatuletea mafanikio ndani ya wizara yetu ni kufanya kazi kwa bidii,
kufanya kazi kwa kushirikiana na tukifanya hivyo hakika tutapendana na kuzidi kufanikiwa,”
alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, hapendi kuona mtumishi yeyote ananyanyaswa kwa kutopewa haki zake
au kucheleweshewa pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo malipo mbalimbali ya watumishi
wanayodai, na endapo yatatokea hayo watumishi hao wamletee kero zinazowakabili ofisini
kwake na kwa kushirikiana na katibu mkuu wa wizara hiyo watazitatua.
“Utumishi wa umma naujua, na pia nimepitia manyanyaso kadhaa mpaka leo nimefikia hapa
kutokana na historia yangu, kwanini tusipendane?, kwanini tunyanyasane?, kwanini
tusishirikiane?, ni tabia mbaya na inatakiwa kulaaniwa kwa baadhi ya wakuu wa idara na vitengo
pamoja na wengineo ambao wanatabia ya kunyanyasa watumishi waliochini yao,” alisema
Lugola.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kwa Waziri Lugola, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja
Jenerali, Jacob Kingu pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima, kuzungumza na
watumishi wa Wizara hiyo tangu walipoteuliwa miezi kadhaa iliyopita, walitaka kujuana zaidi na
watumishi wa wizara hiyo pamoja na kujua changamoto zao zinazowakabili.
Toggle screen reader support
No comments:
Post a Comment