Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei (kulia) wakati alipowasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza, Oktoba 1, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambaba.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akipokea sehemu ya vitendea kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei wakati alipowasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza, Oktoba 1, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, (wa pili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Huduma Shirikishi), Dora Ngaliga (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu, Timoth Fasha (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambaba, baada ya kuwasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza, Oktoba 1, 2018.
No comments:
Post a Comment