ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 20, 2018

BOT YAFANYA OPARESHENI MAALUMU YA UKAGUZI NA UDHIBITI WA MADUKA YA KUBADILISHIA FEDHA

Gavana wa Benki Kuu Nchini Tanzania Profesa Florence Luhoga akitoa ufafanuzi kuhusiana na ukaguzi na udhibiti wa biashara haramu ya fedha za kigeni na ukiukwaji wa sheria katika kuendesha biashara ya ubadilishaji fedha yaani (Bureau de Change)Picha na Vero Ignatus

Na Vero Ignatus, Arusha
Benki Kuu ya Tanzania imeendesha operesheni ya kushtukiza ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha(Bureau de Change) na kubaini baadhi ya maduka bubu yasiyokuwa na leseni ambayo yalikuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha Gavana wa Benki kuu nchini profesa Florence Luoga amesema kuwa zoezi hilo liliratibiwa na kitengo cha ukaguzi cha Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kisheria

Aidha amesema kuwa Operesheni hiyo ni ya tatu kufanyika ambapo uchunguzi wa kina wa miezi sita umebaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha kinyume cha sheria na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni, utakatishaji fedha, hususani kupitia maduka ya kubadilisha fedha

Aidha Luhoga amesema kuwa BOT imechukua hatua kusitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha kwa takribani miezi mitatu, na wale wote watakaokutwa na makosa ya uvunjaji sheria,leseni zao zitafutwa na hawataruhususiwa kufanya biashara hiyo tena 

'' Katika kipindi hikiwakati wa kesi zao zinashughulikiwa kisheria na ili kuzuia kuendesha biashara haramu leseni zao zinasitishwa na wanatakiwa kuzirudisha Benki kuu mpaka kesi zao zitakapokamiika baada ya hapo taratibu mpya zitatumika''


Amesema wale wote ambao wana tuhuma za kukiuka sheria katika oporesheni mbili zilizopita na kufikishwa polisi, wanatakiwa kurejesha leseni zao BOT mara moja ambapo leseni hizo zitasitishwa hadi pale kesi zao zitakapokamilika

Uchunguzi uliofanywa na BOT umebaini waendeshaji wengi wa maduka ya kubadilisha fedha hawajakidhi vigezo vyote japokuwa leseni zilitolewa kwao baada ya taarifa kupitoshwa 

'' Hao wote watapewa notisi ya kusitisha leseni na maduka yao kufungwa, yeyote anayejua kuwa upatikanaji wa leseni yake unadosari anashauriwa kurejesha kwa hiari''alisema Gavana

Pia amewataka wale wote wanaoendesha maduka ya kubadilisha fedha bila leseni au kwa kutumia leseni zisizo za kwao kufunga maduka hayo mara moja kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria 

Aidha Gavana Luhoga amesema kuwa BOT haitazungumza chochote kwa sasa, mahojiano na wahusika yanaendelea na wale watakaokutwa na tuhuma za ukiukwaji wa sheria watashughulikiwa kufuatana na taratibu za kisheria 

Gavana amesema kuwa juhudi za kitengo cha ukaguzi kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika operesheni mbili zilizopita kwani imegundulika kuwa kuna mtandao mpana na madhubutu wa shughuli hizo na ambao ulilenga kuhakikisha shughuli za udhibiti hazifanikiwi. 

Ameeleza kuwa ukaguzi huo wa kushtukiza ulifanyika jana Jijini Arusha mara baada ya mashauriano na wataalam kwa kushirikisha vyombo vya upelelezi, na usimamizi ilionekana ili kufanikisha zoezi hilo wahusika wote wadhibitiwe kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi ,ambapo ilihusisha maofisa wengi kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi 

"Baadhi ya washiriki katika zoezi hilo ni askari wa jeshi la wananchi Tanzania wakiwa katika sare zao bila silaha, tulilazimika kutumia Jeshi la wananchi kwenye operesheni kwani askari wengi wa jeshi la polisi walikuwa kwenye kusimamia usalama katika vituo vya mitihani ya kidato cha pili iliyokuwa ikiendelea''alisema Luhoga

Gavana Profesa Florence Luhoga amesema BOT inayo hifadhi ya pesa za kigeni ambazo zinaweza kuendesha nchi ndani ya miezi mitano na siyo kwamba kuendesha kwao ukaguzi ni kutokana kupungukiwa na fedha kama inavyodhaniwa lahasha,bali Tanzania ina hifadhi ya fedha za kigeni ni Afrika.

No comments: