Advertisements

Sunday, November 18, 2018

MAWAZIRI WAKUTANA KUJADILI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA PAMOJA YA UJENZI WA UCHUMI WA VIWANDA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa Sekta za uchumi walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 17, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda (Mb) akielezea utekelezaji wa Wizara yake wakati wa kikao hiko walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Kikao hiko cha Mawaziri wa Sekta za kiuchumi walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (Mb) akielezea umuhimu wa kila Wizara kutekeleza majukumu kwa haraka ili kutimiza malengo wakati wa Kikao hicho.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ezamo Maponde akiwasilisha mada kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Sekta za Kiuchumi walipokutana Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mita Waitara (Mb) akichangia mada wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi wakimsikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda Jijini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi wakimsikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walipokutana kujadili utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustine Kamuzora akielezea jambo kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi wakati wa kikao hicho. (Kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula. (Kushoto) ni Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Buchweshaija
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na baadhi ya Mawaziri (kushoto) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Isack Kamwelwe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi mara baada ya kumaliza majadiliano ya utekelezaji wa Programu ya pamoja ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

No comments: