ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 20, 2018

TANZANIA YAISHUKURU UNESCO, KOREA KUSINI KWA MRADI WA UFUNDI STADI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (katikati) akiwasili na kupokelewa na Mkuu wa kitengo cha Elimu katika shirika la UNESCO, Bi. Faith Shayo (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi iliofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Ofisa Balozi mdogo wa Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha Elimu katika shirika la UNESCO, Bi. Faith Shayo (kushoto) wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa mradi wa BEAR ll, kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim.
Mratibu wa mradi wa Bear II nchini, Bi Andulile Daudi (kushoto) akibadilishana mawazo na Ofisa aneyshughulikia uratibu wa ushirikiano ufundi stadi kati ya Tz na Ujerumani kutoka Handwerkskammer jijini Hamburg, Bw Frank Glucklich (katikati) pamoja na Mshauri kutoka Handwerkskammer jijini Hamburg, R. Nicolas Udewald wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Elimu katika shirika la UNESCO, Bi. Faith Shayo akitoa neno la ukaribisho kwa meza kuu na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mratibu wa mradi wa BEAR ll, kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Whan Sik Kim, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo, Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, Ofisa Balozi mdogo wa Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An pamoja na Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Noel Mbonde akizungumzia mradi wa BEAR II kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Ofisa Balozi mdogo wa Ubalozi wa Korea nchini, Bi. Jiin An akitoa salamu za serikali ya Korea Kusini kwa niaba ya Balozi wa Korea Kusini, Mh. Geum Young Song wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi wa BEAR II kutoka ofisi za Unesco Nairobi, Bw.Teeluck Bhuwanee akitoa neno kwa niaba ya Unesco wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Injinia Enock Kayani kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akiwasilisha mpango kazi wa mwaka mmoja ulioandaliwa na kamati ya kifundi wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau kutoka MoEST, Wizara wa Kilimo, UNESCO, NACTE, TCCA, ATE, VETA pamoja wadau wa maendeleo walioshiriki halfa ya kufunga mafunzo ya siku tatu ya mradi wa Bear ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo pamoja na washiriki wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa BEAR ll na warsha ya kiufundi yaliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja. BEAR ll ni mradi wenye lengo la kuleta elimu bora kwa mataifa ya Afrika.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo ameshukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) na Ubalozi wa Korea Kusini kwa kufanikisha warsha inayoandaa mpango kazi kwa walimu na wadau wanaosimamia mafunzo ya ufundi stadi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya mradi wa Bear ll Katibu Mkuu huyo alisema wakati taifa linaelekea katika uchumi wa viwanda mradi huo na mafunzo yake ni kitu muhimu sana.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalijadili namna ya kufikisha elimu ya ufundi stadi inayooana na mahitaji halisi ya nguvu kazi katika jamii.
Mafunzo hayo yalilenga kutambua na kusaidia kufanikisha malengo matatu ya matumizi ya ufundi stadi yanayozingatia mahitaji ya uchumi, kuboresha mafunzo ya ufundi stadi kwa wateja na kuboresha hali ya uelewa wa ufundi stadi miongoni mwa vijana na wananchi.
Katibu mkuu huyo alisema kwamba serikali inajivunia hatua iliyofikiwa ya mradi huo wa Bear ll ya uandazi wa mpango kazi wa mwaka mmoja na wa miaka mitatu ambao kwa sasa unasubiri kamati ya wizara kuupitia na kuubariki.
Alisema kwamba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha kwamba mradi huo wa Bear ll unatekelezwa na kutoa matunda yanayotarajiwa.
Katika warsha hiyo mada kadhaa ziliwasilishwa ikiwamo mkakati wa UNESCO kuhusu ufundi stadi na historia ya mradi wa Bear II ambao unapoletwa nchini Tanzania upo katika awamu ya pili.
Mradi huo wa Bear ll unafanyika katika nchi tano zikiwamo Tanzania na Uganda katika awamu yake ya pili. Nchi zingine ni Ethiopia, Kenya na Madagascar.
Kwa mujibu wa taarifa za kitafiti kuna malalamiko kwamba wahitimu wa ufundi stadi wanashindwa kwenda sanjari na matakwa ya shughuli zao katika viwanda.
Mradi huo wa dola za Marekani milioni 1.56 unatarajiwa kugusa mamlaka mbalimbali za mafunzo nchini yakiwemo mafunzo ya ufundi stadi zitakazowezesha wafundishaji kutoa mwanga unaotakiwa kwa mafundi stadi. Mamlaka hizo ni pamoja na TCU, Nacte, Baraza la Ithibati nakadhalika.
Wakati wa uzinduzi wa mradi huo Balozi wa Korea Kusini Geum- Young alisema taifa lake litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba linawezesha elimu ambayo ni msingi mkubwa wa maendeleo ya viwanda.
Naye Mkuu wa kitengo cha cha elimu katika shirika la UNESCO Faith Shayo alisema kwamba lengo kubwa la mradi huo ni kuboresha mafunzo ya ufundi nchini na kuweka uwiano wa masomo hayo ili kuhakikisha kwamba yanachangia katika ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Mratibu wa BEAR II Bw.Teeluck Bhuwanee alisema ni matumaini yake kwamba ushirikiano kati ya serikali, Korea Kusini na Unesco utasaidia kuboresha elimu ya ufundi nchini.

Kuzinduliwa kwa BEAR II kunaashiria utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kuendeleza utaalamu (NSDS) kuanzia mwaka 2016/17 hadi 2025/26 wenye lengo la kuwa na wafanyakazi wataalamu na wenye ushindani.

No comments: