ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 21, 2018

WAJASIRIAMALI 250 KUSHIRIKI MAONYESHO YA SIDO KANDA YA KASKAZINI JIJINI TANGA

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza kuhusiana na maonyesho hayo kushoto ni Mhasibu wa SIDO mkoani Tanga Janeth Kiwale
 Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga  Gladness Foya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kesho na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Mhasibu wa SIDO Mkoani Tanga Janeth Kiwale.
Sehemu ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia mkutano huo

ZAIDI ya wajasiriamali 250 wamekwisha wasili Jijini Tanga kwa ajili ya  maonyesho ya Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO)Kanda ya  Kaskazini yanayotarajiwa kuanza kesho Nov 22 hadi 26 ambapo mgeni anatarajiwa  kuwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda

Hayo yamezungumzwa na Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga  Gladness Foya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya tangamano Jijini hapa  na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Foya alisema maandalizi yapo vizuri na tayari baadhi ya wafanyabaishara  toka Nchini Uganga na Burundi wamekwisha wasili kwa ajili ya maonyesho hayo  ambayo yanajumuisha mikoa ya Tanga,Kilimanjaro.Arusha na Manyara.

“Tumekwisha anza pokea wageni na wapo zaidi ya wajasiriamali 250 wamekwisha  wasili na watatu toka Uganda na watano toka Burundi na tunatarajia kupokea  wageni zaidi katika maonyesho haya”Alisema Foya.

Awali akizungumzia maonyesho hayo Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella  alisema ni fursa kwa Watanzania na wananchi wa ndani ya jiji na nje  kujifunza namna Serikali ya awamu ya tano inavyotekeleza kwa vitendo uchumi  wa viwanda.

Aidha alisema tayari taasisi za kifedha,wamili wa viwanda na wasindikaji  wamekwisha wasili Jijini hapa kwa ajili ya maonyeshoi hayo ambayo  yatawajenga katika nyanja hiyo ya uchumi wa viwanda na ujasiriamali.

“Tunaowageni wengi tumekwisha anza wapokea na zaidi ni fursa kwetu na  wajasiriamali maana watapata muda wa kuuza bishara zao na kuona bidhaa  zinazozalishwa na sido na wanaweza kuomba kutengenezewa labda niseme tu ni  fursa kubwa”Alisema Shigella.

Hata hivyo aliwaomba wafanya biashara kuyatumia maonyesho hayo ili kuweza  kujinufaisha kibiashara na namna ya kuweza kupata bidhaa bora toka shirika  hilo la Sido.

No comments: