Mkazi wa kijiji cha Mangae , kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Anita John akitoa malalamiko yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani ) kuhusu Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika eneo la kijiji hicho kuendesha shughili zao pasipo kuwafidia makazi yao waliyokuwa wakiishi kupisha uchimbaji wake.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisoma baadhi ya nyaraka za Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo na ( wapili kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mohamed Utaly.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( aliyeweka mikono mfukoni) akipewa maelezo na kuangalia mashine za Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( aliyeweka mikono mfukoni) akiteremka chini kutoka kuangalia mashine za Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( mwenye kuvaa shati la madoamadoa ) na ( wa kawanza kulia ) ni Kamishina kutoka Tume ya Madini , Dk Athanas Macheyeki , na ( wapili kushoto ) ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero , mkoani Morogoro , Mohamed Utaly pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wakazi wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wapili kulia ) akiongozwa na Mwakilishi wa Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae , wilayani Mvomero , mkoani Morogoro, Daniel Agustino ( kulia) ambaye pia ni mhasibu wakazi wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo wengine walioambatana na Naibu Waziri ( kati kati mstari wa nyuma ) ni mkuu wa wilaya hiyo , Mohamed Utaly .
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( kulia ) akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae , wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo na ( kati kati mwenye kushika simu) ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( kushoto ) akiwahoji jambo baadhi ya wafanyajkazi waliopo kwenye Menejimenti ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae , wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro wakiongozwa na Mwakilishi wa uongozi wa juu wa Kampuni wake Mwakilishi wa Kampuni ya MMC , Daniel Agustino ( kulia) ambaye pia ni mhasibu wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo .
Wakazi wa vijiji vya Mangae , Msongozi na Mtipule katika kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wakitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani ) kuhusu namna ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika eneo la kijiji hicho isivyowatendea haki kwa kushindwa kwao kuwalipa fidia , kufunga barabara na ajira za upendeleo kwa wageni wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wapili kutoka kulia ) akisikiliza kero na changamoto mbalimbali za wakazi wa vijiji vya Mangae , Msongozi na Mtipule vilivyopo wilaya ya Mvomero , mkoani Morogoro dhidi ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo na ( watatu kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero , Mohamed Utaly na ( wa kwanza kulia anayeandika ) ni Kamishina kutoka Tume ya Madini , Dk Athanas Macheyeki.
Baadhi ya watendaji wa menejimenti ya wafanyakazi wa Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae , wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani ) katika kikao kilichofanyika mara wakati wa kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wapili kutoka kulia ) akiwasalimu baadhi ya wafanyanyakazi na viongozi wa Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero ,Mohamed Utaly.
Na Mwadishi wetu, Morogoro
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Menajimenti ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji ch Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro kusimamisha uchimbaji hadi itakapokamilisha taratibu za kisheria za Serikali zinazosimamia madini pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliohamishwa meneo yao waliokuwa wakiishi.
Biteko alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo kwenye eneo la mgodi huo uliopo katika vijiji vya Mtupule na Mangae na kubaini imekuwa ikeindelea kuchimba madini ya dhahabu kinyume na sheria licha ya kutakiwa kukamilisha kwanza utaratibu waliopewa wa kisheria .
Mbali na hilo , Naibu Waziri alionya na kutoa wito kwa Watanzania wote wanapoamua kuingia mikataba na mikataba ya wachimbaji wadogo ni lazima itambuliwe na serikali kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji sekta ya madini na si vinginevyo.
Naibu Waziri alisema , kufuatwa kwa sheria na utaratibu wa mikataba na wawekezaji wa n je inalenga kuwalinda uwekezaji wao ili baadaye wasione wananyanyaswa pale mikataba walioingia na watu wasio waaminifu inakinzana na sheria mpya ya madini
Hata hivyo alisema , manufaa ya madini kwa wananchi wa eneo hilo hayawezi kupatikana endapo mahusiano kati ya mgodi na wananchi hayatakuwa mazuri na kwamba rasilimali za nchi lazima ziwanufaishe Watanzania wote yakiwemo Madini.
“ Wizara ya Madini inatoa leseni na mwenye leseni baada ya kuipata anapaswa kwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa wilaya husika na mkuu wa wilaya anamtambulisha kwa mtendaji wa Kata hadi Kijiji “ alisema Biteko na kuongeza kusema
“ Kwa pamoja watendaji wa kata na kijiji wataenda kuweka alama ya mipaka eneo la uchimbaji na kukiwa na watu juu ya ardhi na mimea yao hapo mwekezaji atafanya mazungumzo na wananchi ili kuwalipa fidia kulingana na utaratibu wa kisheria wa uthamini kabla ya kuanza uchimbaji ” alisema Biteko.
Naibu Waziri huyo alisema ,kwa mujibu wa sheria hakuna mtu mwenye leseni kuchimba madini bila kumalizana na mtu aliyemkuta juu ya ardhi ,hivyo alimwagiza mkuu wa wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na mamkala zingine kuhakikisha shughuli za uchimbaji hazifanyiki hadi wananchi watakapolipwa fidia zao ikiwa na kukamilisha sheria za madini.
Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo waliokusanyika eneo la mgodi baada ya kuwasili Naibu Waziri kwa nyakati tofauti walitoa malalamiko yao dhidi ya mwekezaji huyo ikiwemo ya kufunga barabara inayiunganisha vijiji vyao na makao makuu ya kata ambayo inapita eneo la mgodi.
Baadhi ya wakazi hao akiwemo Mchungaji wa Kanisa la Methodist, Hilda Ngowi , Anista John , Andrian Soketi pamoja na Karaita Saita kwa nyakati tofauti wakidai mbele ya Naibu Waziri huyo kuwa mwekezaji huo wamewaondoa maeneo hayo bila kuwalipa fidia na kuanza shughuli za uchimbaji wa madini.
Hata hivyo alidai ,baadhi ya wananchi walilipwa fedha kidogo kiwango kinachofikia Sh 500,000 na bati 23 tu jambo ambalo halikuwa la kisheria .
Mchungaji Ngowi ,alilamikia kwa mwekezaji huyo kufunga barabara hali inayowawia vigumu wao kusafiri kutoka upende mmoja wa vijiji hivyo ikiwa ni kwenda kupata huduma za matibabu Zahanati iliyopo makao makuu ya Kata na vijana wazawa kukosa ajira.
Naye mkuu wa wilaya hiyo, Utaly alisema, tayari walianza kuchukua hatua kabla ya ujio wa Naibu Waziri hasa la matumizi ya barabara na kwamba kufuatia maaagizo hayo , Serikali ya wilaya itasimamia utekeleaji wa kuona fidia inalipwa kwa wahusika na barabara inafunguliwa na kuwataka wananchi kufuata utaratibu rafiki utakaowekwa wakati wa kupita eneo la mgodi huo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya MMC , Daniel Agustino alisema kuwa kampuni huyo ilipata usajili wake Novemba 2015 na kuanza shughuli za utafutaji wa nmadini mwaka 2016 katika kijiji cha Mangae , Kata ya Mangae , wilayani Mvomero.
Hata hivyo alisema kuwa, changamoto zote ziliozjitokeza na maelekezo ya Naibu Waziri wa Madini yatatekelezwa kwa haraka ili shughuli za uchimbaji ziweze kuruhusiwa tena kwa manufaa ya Kampuni, jamii na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment