Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akitoa wito kwa wasanii wote nchini kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha, alipokuwa akizindua mfuko huo ambapo amesisitiza kuwa wasanii wa makundi yote wanaweza kujiunga.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza aliyejifunika mgorori mwekundu wa kimasai akicheza na wanakwaya wa jamii ya Kimasai kutoka kanisa la KKKT Meserani alipowasili kuzindua Mfuko wa Mkopo unaoratibiwa na TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) leo Jijini Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) mara baada ya kuzindua Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha,(aliyeketi wapili kulia) ni Rais wa Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) Dkt. Godfrey Maimu.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (nyuma wapili kushoto) akicheza wimbo Hapa Kazi Tu uliyokuwa unaimbwa na Msanii Isack Chalo leo Jijini Arusha,mara baada ya uzinduzi wa wa Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND).
Na Anitha Jonas, WHUSM, Arusha
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa wasanii kujitokeza na kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Jijini Arusha alipokuwa akizindua Mfuko Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND katika Tamasha la Tukuza Festival lililoandaliwa na Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE).
“Tumekuwa tukishuhudia wasanii wengi wenye majina makubwa wakikosa fedha hata za matibabu hili limekuwa ni suala lisilo pendeza hivyo ni vyema wasanii mkajiunga katika mfuko huu ambao utawasadia kupata mikopo yenye riba nafau na bima ya afya kupitia hili mnaweza kujikwamua kiuchumi na kujifunza kuwekeza kwa maisha ya baadae ,“alisema Mhe.Shonza.
Kwa Upande wa Rais wa TAGOANE Dkt.Godfrey Maimu alifafanua kwamba mfuko huo haubagui msanii kwani msanii yeyote anayetaka kujiunga anaruhusiwa kwani lengo la mfuko huo ni kuimarisha umoja wa wasanii na kuhakikisha maisha ya msanii yanaenda kubadilika badala ya msanii kuonekana ni mtu tegemezi na wakuomba kusaidiwa hata kwenda studio kurekodi.
“TAGOANE tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kusaka vipaji vya uimbaji kwa watoto yatima ambapo lengo ni kuwasadia katika kukuza vipaji vyao lakini pia na kuwasimamia masuala ya shule katika kuhakikisha wanapata mahitaji yote muhimu ya shule,”alisema Dkt.Maimu.
Kwa upande wa Katibu Mwenza wa TAGOANE Bw.Silvanus Mumba alieleza kuwa Tamasha hilo kwa mwaka huu limemeendesha Semina ya siku mbili kwa wasanii kuhusu masuala ya Sheria,Sanaa na Ubunifu lengo likiwa ni kumjenga msanii kuendesha shughui zake kwa weledi.
Halikadhalika nae Mmoja wa watoto yatima kutoka Wilaya ya Siha ambaye ni yatima mwenye kipaji cha kuimba nyimbo za injili Witness Justine aliushukuru uongozi wa TAGOANE kwa kumuahidi kumpeleka studio kurekodi nyimbo zake pamoja na kuzitangaza nyimbo hizo pia aliwashukuru kwa kujitoa kumsomesha.
No comments:
Post a Comment