ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 31, 2018

TAARIFA YA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 katika kipindi cha Julai-Novemba, 2018), ambapo alisema Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi tano zinazokua kwa kasi kiuchumi Barani Afrika, wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, akielezea jambo kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019, kwa kipindi cha Julai - Novemba, 2018, katika ukumbi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Wadau wengine wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019, kwa kipindi cha Julai - Novemba, 2018, wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waandisi wa Habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango,  kuhusu  Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019, kwa kipindi cha Julai - Novemba, 2018ambapo alisema katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 ikilinganishwa na asilimia 6.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2017. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari Jijini Dodoma, kuhusu ufadhili wa wahisani ambapo alisema Wahisani wengi wanamasharti magumu hivyo akasisitiza umuhimu wa  wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kujitegemea. 
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb), (katikati), wakifuatilia kwa makini baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari kuhusu taarifa iliyotolewa ya Hali ya Uchumi wa nchi na Utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments: