Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba Dr. Sira Ubwa Mamboya akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akihutubia katika katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Pro. Makame Mbarawa, Katika picha ya pamoja na viongozi wengine was serikali wakaribishaji wa hafla ya Uzinduzi wanara wa kuongozea ndege wa Pemba.
Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege Pemba.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi mnara wa kuongozea ndege wa Pemba, baada ya kufanyiwa Ukarabati mkubwa. Hafla hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mgeni rasmi akiwasili Katika hafla ya Uzinduzi mnara wa Kuongozea ndege Pemba.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezindua mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba, Zanzibar.
Mradi huu umegharimiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Prof. Makame Mbarawa amesema mnara huo umezinduwa mara baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ulioanza Novemba 2017 hadi Agosti 2018.
Amesema kuwa mradi huu wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 ni miongoni mwa miradi inayozinduliwa katika wiki ya maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mradi unalenga kuboresha huduma za uongozaji ndege katika uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na kuimaimarisha usalama wa abiria na vyombo vinavyotumia uwanja huu.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba Dr. Sira Ubwa Mamboya ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu inayopelekea kupata matokeo chanya.
"Binafsi sina la kusema leo nimefurahi sana kuona jinsi serikali zetu zinavyopambana kuleta miundo ya kisasa ili kuweza kwenda na teknolojia ya kisasa," amesema.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari amesema ukarabati umefanywa na Kampuni ya kitanzania ya M/s Future Century Limited ambapo kazi zilizofanyika ni pamoja na kubadilisha vioo vinavyozunguka mnara wa kuongozea ndege, kurekebisha paa na kuzuia kuvuja, kuweka vizuizi vya usalama (guard rails) na kuweka upya mfumo wa viyoyozi (Air conditioning), kuweka upya mfumo wa umeme, kuweka upya mfumo wa simu na taarifa za kieleckroniki na kupaka rangi upya.
No comments:
Post a Comment