ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 28, 2019

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ARIDHISHWA NA KASI YA UKALIMISHWAJI WA OFISI YAKE

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akifafanua  juu ya mgawanyo wa  Ofisi kwa    baadhi ya wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi  na wakuu wa vitengo wakati walipotembelea  kukagua  maendeleo ya kazi ya ukamilishwaji wa jengo la awamu ya kwanza  la  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali linaojengwa katika Mji wa Kiserikali  katika Kata ya Mitumba- Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Mwanasheria Mkuu  amesema anaridhishwa  kasi ya kukamilishwa   kwa kazi zilizobaki katika  jengo hilo
 Injinia Mwanadada  Suma Atupele ambaye amekuwa akisimamia kazi  za ujenzi wa Jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  tangu jengo hilo lilipoanza kujengwa akitoa maelezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ujumbe wake namna  Ofisi zitakavyo fanyiwa  mgawanyo ( partitioning).
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi akielezea  kwa  kuchora  ardhini mgawanyo na  matumizi ya sehemu ya eneo la ukubwa wa ekari  karibu tano ikiwamo sehemu ambayo limejengwa jengo la awali   ambalo  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  imepewa na  Serikali katika  Mji wa Kiserikali  Mitumba- Ihumwa.
 Kazi ya uwekeaji  wa (vigae)tiles ukiendelea,  kama inavyoonekana katika  chumba hiki.  
     Kazi ya upakaji rangi nje ya jengo  ikiwa inaendelea kama  inavyoonekana

Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amesema, anaridhishwa  sana   na kasi ya ukamilishaji wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu linalojengwa  katika  mji wa Kiserikali   ulipo katika Kata ya Mitumba- Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma
Jana ( Jumatano) Profesa Kilangi aliwoongoza   Wakurugenzi,  Wakurugenzi  Wasaidizi na Wakuu wa  Vitengo kukagua kazi inayoendelea katika ukamilishaji wa jengo hilo.
“Ninaridhishwa   na ninafurahi sana kwa kasi na kazi nzuri  ya  ukamilishaji wa jengo hili.  Kila ninapofika hapa kwenye site nakuta kazi mpya inaendelea, hongera sana Injinia kwa usimamizi wako  pamoja na timu yako” amesema.
Akiogozwa na Injinia Suma Atupele. Mwanasheria Mkuu na ujumbe wake alipita  na kukagua kila Ofisi huku akitoa maelekezo kwa Naibu Mwanasheria Mkuu na  Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali  Watu juu ya mpangilio na mgawanyo wa Ofisi kwa  kuzingatia  muundo   na majukumu  ya Ofisi.
Katika  maelekezo yake kwa viongozi hao, Profesa Kliangi amesisitiza   katika upangaji  wa Ofisi kuhakikisha kwamba, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi  na   maafisa walio chini yao hasa kutoka Divisheni za   kisheria wanakuwa katika utaratibu wa kuhamia katika jengo hilo pale litakapokuwa tayari kuhamia.
 Baada ya  kukagua maendeleo ya  ukamilishaji  wa jengo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake alipata pia fursa ya kuangalia eneo zima lenye ukubwa wa ekari tano  ambalo limetengwa kwa ajili ya  ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo  kubwa zaidi ambalo litakuwa na uwezo wa kutosheleza watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na matumizi mengine yakiwamo ya ujenzi wa Chuo  maalum kitakachokuwa kikitoa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali.

No comments: