ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 8, 2019

KIKWETE ATEMBELEA SEKONDARI MBOGA

Na Karim Juma - Mboga -chalinze
RAIS Mstafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekagua maendeleo ya shule ya sekeondari  Mboga na kujiridhisha kwa utendaji wa bodi ya shule hiyo na  bodi ya shule hiyo  kuhitajika kuachia madaraka kufuatia na waraka uliotolewa na Wizara ya elimu  kwa shule za sekondari .
Dkt. Kikwete amesema kwamba  uchagauzi wa bodi mpya  ufuate maelekezo kama yaliyotolewa kwenye waraka huo na sio kumchagua mtu kwa umarufu alionao, Hata hivyo  kikwete aliomba wanafunzi na walimu  watunze shule kwa kuwa ni ya kisasa sana na bado itaendelea kuwekezwa kwa kupata elimu ya kidato cha tano na cha sita.

 Amesema kuwa kwa wakati huu wakiendelea na utengenezaji wa majiko ya kupikia na wamepanga kujenga bwalo  la  chakula kwa wanafunzi pamoja na sehemu ya kuhifadhia chakula.

   Pia Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amesema ameridhishwa na  uwajibikaji, utendaji kazi kwa kuonesha kauli mbiu ya hapa kazi inatekelezwa hasa kwa  bodi ya shule kujinyima posho ili shule iweze kuwa salama na kuweza kukamilika pamoja  na kupata watendaji wa kufundisha vijana kwa ufasaha.
              Ridhiwani amesema ni wakati sasa kwa Halmashauri ya Chalinze kutumia pesa za ndani kuweza kuwapa posho walimu wa kujitolea kwa kuwa kuna uhaba wa walimu wasayansi na kwa hali ya sasa ya dunia inanyoendeleha lazima kupate wataalamu wa mambo ya teknolojia.

No comments: