Gari waliopanda wataalamu kutoka Ofisi ya mkoa wa Rukwa likiwa limekwama huku wataalamu hao kwa ushirikiano na wajumbe wa Kamati ya ulinzi ya Mkoa wakijaribu kulikwamua kutoka kwenye tope zito wakati wakitokea kijiji cha Jengeni Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo.
Gari la Mkuu wa Wilaya ya Kalambo likiwa limekwama na kujaribu kukwamuliwa kutoka kwenye tope zito liliosababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha hali ya barabara kuwa mbaya.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivuka daraja la miti kuelekea katika kijiji cha Jengeni, Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo. daraja hilo ndilo wanalotumia wananchi katika shughuli zao za kila siku hasa wakati wa masika. Chini ya daraja hilo unapita mto China.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akivuka daraja la miti lililojengwa juu ya mto Kalambo kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe ambacho kipo karibu na Kijiji cha Jengeni alipokwama kuendelea na safari kwa siku ya kwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivushwa katika daraja la miti na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nondo Robert Sikombe kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe ili kukutana na wananchi hao na kufahamu changamoto mbalimbali wanazokumbana nanzo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akivuka daraja la miti katika mto china ili kufika katika kijiji cha Jengeni na kuelekea katika kitongoni cha Kamleshe kijiji cha Nondo, Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivuka daraja la miti kuelekea katika kijiji cha Jengeni, Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo. daraja hilo ndilo wanalotumia wananchi katika shughuli zao za kila siku hasa wakati wa masika. Chini ya daraja hilo unapita mto China.
Kaimu RAS - Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya akivuka daraja la miti kuelekea katika kijiji cha Jengeni. kuonana na wananchi kisha kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe kilichopo kijiji cha Nondo, Kata ya Mpombwe, Wilayani Kalambo.
No comments:
Post a Comment