Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau(kushoto) akizungumza na Wanahabari jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Kulia ni baadhi ya Wanahabari wa jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu huyo.Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura(kushoto) akizungumza na Wanahabari jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Kulia ni baadhi ya Wanahabari wa jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu huyo.Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
Wanahabari wa Jijini Mwanza wakifuatili kwa makini mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI..Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
WIZARA ya afya kwa kushilikiana na Mradi wa USAID Tulonge
Afya fhi 360 wametoa mafunzo kwa wanahabari jijini Mwanza
juu ya utoaji habari wakati wa maandalizi ya uzinduzi wa
Majukwaa mawili ya mawasiliano ya afya kwa watu wazima
litakaloitwa “NAWEZA” na kwa vijana “SITETELEKI” ili
kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania
uwezo na kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta
matokeo chanya.
Mafunzo hayo yalifanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki
katika Hotel ya Gold Crest ambapo yalipata mwitikio mkubwa
na ulewa mzuri kwa wanahabari waishio jijini Mwanza.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu mambo ya Afya
kutoka Wizara ya Afya na USAID Tulonge Afya fhi 360.
NAWEZA ni jukwaa litakalolenga kuwafikia wananchi tofauti
tofauti itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanania
wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya
maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama
makundi mengine hususani watu wazima.
SITETELEKI ni jukwaa litakalolenga zaidi kuwafikia Vijana
wenye umri kati ya 15 – 24, wanaokabiliwa na changamoto
nyingi za malengo ya maisha.
No comments:
Post a Comment