Wednesday, March 6, 2019

WANAWAKE CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MOROGORO WAAZIMISHA SIKU YA MWANA MKE DUNIANI KWA KUANGAZIA CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI WANAFUNZI WA KIKE.

 Baadhi ya wanafunzi wa sekondari zilizo karibu na chuo kikuu cha Mzumbe wakiwa katika maandamano ya kusherehekea siku ya wanawake duniani.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro, akipokea maandamamo ya wanawake wa chuo kikuu cha Mzumbe, pamoja na wanafunzi wa kike wa shule ya Adriani mkona na Mongola sekondari.



Umoja wa wanawake wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro wamedhamiria kuwakomboa  wanafunzi wa kike wanao soma shule za sekondari zinazozunguka chuo hicho kwa kuwajengea mabweni ili kukuza kiwango cha elimu.

Wanawake hao wametoa ahadi hiyo wakati wakisherehekea siku ya wanawake duniani ambapo wameeleza kuwa sababu ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na changamoto nyingi zinazo wakabili wasichana na ikiwemo vishawishi vinavyosababisha mimba za utotoni jambo linalipelekea wanafunzi wengi kukatisha masomo yao.
                 
Miongozni mwa shule ambazo zinazunguka chuo hicho cha Mzumbe ambacho ndio kinaongoza kwa ubora nchini ni pamoja na shule ya sekondari mongola, Adrian Mkoba, na kipela pamoja na shule ya msingi Mzumbe.


Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila terehe nane ya mwezi wa tatu kila  mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Fikiri sawa, jenga uwezo na kuleta maendeleo endelevu.
 Mgeni resmi katika mahadhimisho hayo, Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe.
 Mgeni resmi katika mahadhimisho hayo Bi Enedy Mwanokwate ambaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akiangalia maonyesho ya bidhaa ya vitenge vya batiki vinazozalishwa na wajasiliamali wanawake wa kata ya bibwa manispaa ya morogoro
 Prof Aurelia kamuzola akitoa mada ya kuwahamasisha wanawake kujitambua na kuwa na hamasa ya kufikia malengo katika hafla ya kushrehekea maadhimisho ya siki ya wanawake duniani yaliyofanyika katika chuo kikuu cha mzombe mkoani morogoro.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe za siku wa wanawake duniani ambaye pia ni kuu wa kitengo cha maendeleo ya jinsia chuo kikuu cha mzumbe Dr Elizabeth Genda akitoa ahadi ya kujenga mabweni ya wasichana wa shule za sekondari zinazo zunguka chuo hicho.

   Mwakilishi wa mgeni rasmi   Bi Enedy Mwanokwate akipokea picha cha mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina chonjo iliyochorwa na mmoja ya wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha mzumbe katika hafla ya kusherehekea siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika chuo hicho.



                                

No comments: