Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza na wafanyakzi wa banki hiyo, wateja, wafanyakazi wa Ubalozi wa China na kumkaribisha Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke kutoa neno la ufunguzi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akingumza wakati wa ufunguzi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizoandaliwa na benki hiyo zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akinyoosha bendera kuashiria ufunguzi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakishiriki kwenye mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered, wafanyakazi wa ubalozi wa China Nchini Tanzania pamoja na wadau mbalimbali wa Benki hiyo wakishiriki kwenye mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kwanza kutoka China Henry Li akimaliza mashindano ya mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen akimaliza mashindano ya mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akimvalisha medali mshindi wa kwanza anatoka China Henry Li wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akimpa zawadi mshindi wa pili kutoka Uganda Herman Kambugu wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni mshindi wa kwanza kutoka China Henry Li na wa kanza kulia ni mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akimpa zawadi mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke (kushoto) akipiga makofi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani(kulia) mara baada ya kutoa zawadi za medali wa washindi wa wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground jijini Dar es Salaam. katikati ni Mshindi wa kwanza anatoka China Henry Li akionesha tuzo, wa pili kulia ni Mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen na wa pili kushoto ni Mshindi wa pili kutoka Uganda Herman Kambug.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanayakazi wa Ubalozi huo pamoja na wateja wa Benki ya Standard Chartered wa nchini China leo wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
BENKI ya Standard Chartered imesema kazi yake kubwa nchini ni kuwezesha Tanzania kufanya biashara yenye faida na taifa la China kupititia mkakati wa Belt and Road. Benki hiyo imesema ikiwa na wateja 100 wa China (makampuni yenye nguvu) wao wanawezesha wananchi wa Tanzania na serikali kufaidika na biashara na China.
Kauli hiyo imetolewa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw.Sanjay Rughani akizungumza katika mashindano ya Belt and Road yaliyofanyika jana alfajiri.
Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano yanayoendeshwa kwa siku 90 duniani kote. Tanzania ikiwa ni ya 33 kufanya tukio hilo kati ya nchi 44.
Mashindano hayo yaliyofanyika Green Ground, Oysterbay yaliyojulikana kama Belt and Road Relay Race Tanzania washindi walikuwa Henry Li kutoka China aliyeshika nafasi ya kwanza, Herman Kambugu kutoka Uganda aliyeshika nafasi ya pili na Jack Messen aliyeshika nafasi ya tatu akitokea Uingereza. Rughani alisema kwa mwaka jana benki hiyo ilileta biashara ya dola za Marekani milioni 100 nchini Tanzania na kwamba benki hiyo ndiyo inayoongoza kwa kuwezesha biashara kati ya Tanzania na China.
Aidha alisema kwa mwaka jana waliwezesha kujengwa kwa viwanda viwili ambavyo wawekezaji ni kutoka China, viwanda ambavyo vimeajiri watanzania 3,000. Alisema katika mkakati wa ukanda wa hariri, benki hiyo inafanya juhudi kubwa za kuwezesha Tanzania inanufaika kibiashara na China.
"Tunataka watanzania waende katika dunia, wafanyabiashara wa hapa waende China" alisema Rughani na kuongeza kuwa ni lengo lao kuhakikisha kwamba wanaitangaza Tanzania.
Aidha katika mkakati huo alisema kwamba wana dawati maalumu linaloshughulikia Wachina na wafanyabiashara wanaotaka kufanyabiashara na China.
Mbio hizo za jana ni sehemu ya mbio za siku 90 zinazofanyika katika nchi 44 miongoni mwa nchi zilizomo katika mkakati huo wa Belt ulioanzishwa na China mwaka 2013 kwa ajili ya kuboresha biashara na maendeleo ya jamii mbalimbali duniani kwa ushirikiano wa karibu na China.
Nchi hizo zimo za bara la Amerika, Ulaya na Afrika na Asia.
Mbio hizo za kuamsha uelewa miongoni mwa wadau na wateja wa benki hiyo zilizinduliwa Februari 14 mjini Hong Kong kwa mbio za marathon zilizoshirikisha watu elfu 74. Aidha mbio hizo zitamalizikia nchini China Mei 11 wakati wa jukwaa la washiriki wa mkakati huo wa Belt and Road.
No comments:
Post a Comment