ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 10, 2019

WAZIRI LUGOLA AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI WA JESHI LA POLISI, CHUO CHA POLISI MOSHI (CCP)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati wa sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo ya askari wapya wa Jeshi la Polisi katika shule ya Polisi Moshi CCP Mkoani Kilimanjaro, leo. Jumla ya askari 871 wamehitimu mafunzo ya hayo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP Ahmed Msangi alipokua akiwasili katika viwanja vya Shule ya Polisi Moshi CCP wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya askari Polisi 871 waliohitimu mafunzo yao leo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwasili na Msemaji katika viwanja vya Shule ya Polisi Moshi CCP wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya askari Polisi 871 waliohitimu mafunzo yao leo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akikagua gwaride la askari waliohitimu mafunzo ya awali ya askari Polisi katika Shule ya Polisi Moshi CCP. Askari 871 wamehitimu mafunzo hayo yaliyofungwa rasmi leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimkabidhi kirungu cha heshma askari wa kike, mmoja kati ya askari 12 waliofanya vizuri zaidi katika mafunzo ya awali askari Polisi. Mafunzo hayo yamefungwa leo rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola katika viwanja vya Shule ya Polisi Moshi CCP.
Askari wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Uhalifu (SUT) kikipita kwa mwendo wa kunyakua wakati wakifanya onesho maalum wakati wa kufugwa kwa mafunzo ya awali ya askari Polisi katika Shule ya Polisi Moshi CCP. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola alifunga rasmi mafunzo hayo na askari 871 walifanikiwa kimaliza mafunzo.
Askari wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Uhalifu (SUT) wakiwa katika silaha ya kivita aina ya (fourteen) wakati wakifanya onesho maalum wakati wa kufugwa kwa mafunzo ya awali ya askari Polisi katika Shule ya Polisi Moshi CCP. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola alifunga rasmi mafunzo hayo na askari 871 walifanikiwa kimaliza mafunzo. Picha Na Jeshi la Polisi.

No comments: