ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 5, 2019

MADIWANI WA MANISPAA WAFANYA ZIARA YA KATA KWA KATA KUTEKELEZA ILANI YA CCM

Naibu meya wa manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Ryata akihutubia wananchi wa kata ya Mwangata wakati wa ziara ya kimkakati ya madiwani wa CCM manispaa ya Iringa
 Katibu wa itika na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akiwa na mwenyekiti wa vijana wa wilaya ya Iringa mjini Salvatory Ngerera wakati wa ziara ya madiwani wa CCM katika kata ya Mwangata
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kata ya Mwangata manispaa ya Iringa kuwasikiliza viongozi mbalimbali waliojitokeza siku hiyo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MADIWANI wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa wameendelea na ziara ya kuelezea kazi za kimaendeleo ambazo wamezifanya toka wachaguliwe kuwatumikia wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara diwani wa kata ya mwangata manispaa ya Iringa Nguvu Chengula aeleza kazi za kimaendeleo katika sekta ya afya,miundombinu na elimu alizozifanya katika kata hiyo toka achaguliwe kuwa diwani.

“Nilipoingia tu madarakani nilifanyikiwa kukarabati barabara kumi na moja za mitaa ya kata ya Mwangata nilikuwa naona wananchi wachangishana fedha kwa ajili ya kukarabati barabara hizo ndio maana niliamua kuhakikisha barabara hizo zinapitika kilahisi ili kurahisisha shughuli za wananchi zinaendelea vizuri” alisema Chengula

Chengula alisema kuwa amefanikiwa kuboresha majengo ya shule za Mawelewele na Kigamboni zilizopo katika kata hiyo kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi waliopo katika kata hiyo 

“Nampongeza sana father Ulungi na wananchi kwa kutuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Mawelewele lakini mimi kama diwani nikachangia mifuko mia thelathini (130) kwa ajili ya ujenzi huo” alisema Chengula

Aidha Chengula amesema kuwa sekta ya afya imeimalika vilivyo kutokana na kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora kwenye hospital ya Frelimo.

Kwa upande wake naibu meya wa manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi Joseph Ryata amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya uchumi ili kukuza ukchumi kwa wananchi na kuleta maendeleo kwa taifa.

Ryata alisema kuwa watahakikisha barabara  zote za manispaa ya Iringa zinapitika kirahisi ili kuhakikisha kuwa zinapitika na zinakuwa rafiki kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao.

“Wananchi tusipokuwa na miundombinu bora ya barabra hatuwezi kufanya biashara na kupata maendeleo yanayaotakiwa hivyo ni lazima tuwasimamie viongozi wetu wa serikali kuhakikisha barabara zote zinapitika bila kuwa na vikwazo kwa wafanyabiasha na wananchi kwa ujumla” alisema Ryata

Ryata aliongeza kuwa madiwani wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasimamia vilivyo ujenzi wa gorofa katika maeneo ya standi ilipokuwa tembo bara na kuboresha kwa kuujenga upya ukumbi wa Community center ulipo katika kata ya Kitanzini Miomboni na kujenga hoteli ya kitalii katika kata ya Gangilonga.

“Tukiboresha miundombinu hiyo yote na kujenga majengo ya kibiashara yatatusaidia kukuza uchumi wa wananchi wa manispaa ya Iringa na nje ya manispaa ya Iringa hivyo mipango hii inasimamiwa vilivyo na madiwani wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa” alisema Ryata

Ryata aliwataka wananchi wa manispaa ya Iringa kuhakikisha wanaendelea kuwachagua viongozi wa chama cha mapinduzi ili waweze kusaidia kuleta maendeleo kwa haraka na ubora unaotakiwa tofauti na viongozi wengi wa upinzani  hawana hoja za kiuchumi.

Naye diwani wa kata ya Ruaha Tandesi Sanga alisema kuwa wamefanikiwa kuboresha miundombimu ya sekata ya afya,elimu pamoja na miundombinu ya uchumi kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanafanya kazi za maendeleo bila ya kuwa na usumbufu wowote ule.

“Nyie mashaidi toka nimekuwa diwani wa ccm tumefanikiwa kuboresha sekta ya elmu kwa kuboresha miundombinu ya majengo ya shule zetu za sekondari na msingi na zahanati zetu tumeziboesha mno hivyo lazima tufanye kazi kama Rais wetu anavyotutaka” alisema Sanga

No comments: